WATUMISHI WAHIMIZWA KUKAA KWENYE MAENEO YA VITUO VYA KAZI PANGANI


Viongozi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Pangani Mkoani Tanga pamoja na watendaji wa serikali wa Halmashauri hiyo leo wamefanya kikao cha majumuisho ili kujadili changamoto za kiserikali zilizoibuliwa katika ziara za kila kata iliyofanywa na mwenyekiti wa chama hicho. akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Pangani, Katibu wa chama cha CCM wilayani humo bwana Charles Charles amesema kuwa kikao hicho kinatoa nafasi kwa watendaji wa serikali kutoa majibu ya hoja zilizoibuliwa. akiwasilisha changamoto hizo bwana charles amesema kuwa miongoni mwa yaliyoibuka ni pamoja na migogoro ya Ardhi, maji, elimu pamoja na suala la watumishi kukaa nje ya vituo vyao vya kazi jambo ambalo mwenyekiti wa chama hicho alilipiga marufuku mara baada ya kuchaguliwa.
kuna watu hawajarudi kwenye vituo vyao vya kazi bado mtu anafanya kazi sehemu fulani halafu anakaa kwingine lakini wananchi wetu wanakaa kule ambapo wewe unakimbia unasema umeme hakuna
amesema Bwana Charles charles ambaye ni Katibu wa CCM Wilayani humo. Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo bi zainabu abdala issa mbali na kupongeza juhudi za viongozi hao amesema kuwa kama serikali ya halmashuri wamepiga hatua katika utekelezaji mipango mbalimbali iliyoanisnishwa katika maelekezo yaliyoafikiwa na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizoibuliwa "mwaka wa fedha uliopita tumeletewa milioni mia tano kwenye miradi ya maji lakini huu uliopita tumeletewa Bilioni tatu kwenye mirad ya maji Mheshimiwa Mbunge amejitahidi kutatua changamoto ya maji , kama yapo mapungufu mapungufu hayawezi kukosekana haswa katioka sehemua ambayo watendaji tuko wengi na tunatofautiana" Amesema Bi Zainab Abdallah
<b>changamoto nyingine ni changamoto ya uvuvi wavuvi hawa wengine wanategemea uvuvi lakini mara wamekamatwa mara sijui nyavu hizi sizo kwa hiyo changamoto hii ya uvuvi tutakuja tuimalize
ameongeza Bi Zainab Abdallah Pia mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya pangani bwana ISAYA MBENJE amewataka watumishi wa umma kuyafanyia kazi maelekezo waliyopewa ilikuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa wananchi wa pangani. Kikao kikao hicho cha majumuisho kimewakutanisha viongozi mbali mbali wa chama cha mapinduzi kuanzia ngazi ya kijiji ,watendaji wa halamashauri pamoja na wakuu wa idara ikiwa ni kutathmini utekelezaji wa ilani ya chama hicho

No comments

Powered by Blogger.