WAKULIMA NA WAFUGAJI WASHINDWA KUFIKIA MUAFAKA PANGANI


Wananchi wa kijiji cha MADANGA Wilayani PANGANI Mkoani Tanga leo wamekutana katika mkutano wa kujadili changamoto na migogoro iliyopo baina ya wakulima na wafugaji. Wakizungumza katika mkutano huo baadhi ya wananchi hao wameelezea vijiji jirani ambavyo ni JAIRA na KIMANG’A kwamba wafugaji wake wamekuwa wakiingiza mifugo yao katika mashamba yao jambo linalopelekea migogoro ya mara kwa mara kati yao na wafugaji. Mkutano huo uliowakutanisha viongozi wa pande zote tatu yaani KIMANG’A, JAIRA na MADANGA haukufikia muafaka ambapo baadhi ya wananchi wa Madanga wametoa mapendekezo kuwa endapo mifugo hiyo wakiikamata ndani ya mashamba yao igawanywe nusu kwa nusu ama waondolewe kabisa kijijini ili kukomesha migogoro hiyo Kwa upande wake Afisa Tarafa Kata ya Madanga amewasihi wananchi wa kijiji hicho kuwa watulivu ili kufuata taratibu zitakazowawezesha kuweka mikakati ya pamoja kati ya uongozi wa kijiji na wilaya ili kufikia muafaka wa tatizo hilo. Mkutano huo uliotarajiwa kuwakutanisha pamoja wakulima na wafugaji umemalizika bila kufikia makubaliano yenye muafaka kutokana na wafugaji kutojitokeza baada ya kutoa udhuru, hivyo mkutano huo umepangwa kufanyika tena licha ya kutowekwa wazi siku na tarehe rasmi ya kufanyika.

No comments

Powered by Blogger.