MADANGA WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA ILI KUEPUKA MAGONJWA YA MLIPUKO


Wananchi wa kijiji cha MADANGA wilayani PANGANI wametakiwa kusafisha mazingira yanayowazunguka ili kujiepusha na magonywa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu. Hayo yamezungumzwa na Bibi afya wa Kata ya Madanga Bi ZITA MCHOME wakati akizungumza na wananchi wa kijiji hicho na kusema kuwa ni vyema kuchemsha maji ya kunywa, kusafisha mazingira sambamba na vibuyu mchirizi. BI MCHOME amesema kuwa suala la usafi ni muhimu na ambaye hatatekeleza agizo hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Hivi karibuni Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa tahadhari ya kuwepo kwa ugonjwa wa Dengue nchini ambao umebainika katika mikoa ya Dar es salaam na Tanga. Wananchi wa kijiji cha pangani mashariki wametakiwa kujitokeza kwa wingi hapo kesho siku ya jumapili ya tarehe 14/ 4/2019 katika shule ya msingi funguni ili kufanikisha zoezi la uchimbaji wa shimo la karo. Akizungumza na pangani fm radio kwa niaba ya mwenyekiti wa kijiji hicho, mwenyekiti wa kitongoji cha funguni bwana SALIMU KIRABA amesema kuwa wananchi hao ni pamoja na wajumbe wa kamati ikiwemo kamati ya BMU, kamati ya shule na kamati ya VIMC.

No comments

Powered by Blogger.