HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI YANUFAIKA NA AJIRA MPYA ZA WALIMU WA SAYANSI


Halimashauri ya wilaya ya PANGANI mkoani TANGA imeishukuru serikali kupitia ofisi ya rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI kwa kutoa ajira mpya za walimu na kupelekea kupunguza tatizo la upungufu wa walimu hususani wa masomo ya sayansi Wilayani humo. Hayo yamezungumzwa na katibu tawala wa halmashauri hiyo bwana HASSANI NYANGE katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana na kusema kuwa wanaishukuru serikali kwa kutangaza ajira mpya za walimu na kupelekea kupata walimu watano kwa shule za msingi, na nane kwa shule za sekondari ambapo kilio chao kikubwa kilikuwa walimu wa masomo ya sayansi na ajira hiyo imekaribia kutatua tatizo lililokuwepo. Akiendelea kuzitaja shule zilizopata walimu hao ni pamoja na sshule ya sekondari kipumbwi,mwera na funguni na bushiri na kuwaomba wakuu wa idara kuangalia sehemu ambayo ina uhitaji wa walimu wa masomo ya sayansi waelekezwe huko kupitia kibali cha tamisemi. Katika kuhakikisha halmashauri inaborsha elimu wilayani humo pia bwana nyange amesema kuwa wapo katika mchakato wa kuborsha uwepo wa maktaba ili wanafunzi waweze kupata sehemu ya kujisomea. INSERT LIBRALI….. Maktaba hiyo kubwa naya kisasa inatarajiwa kuwepo katika shule ya awali ya sekondari funguni huku katibu tawala huyo akitoa pongezi zake ofisi ua utumishi kwa kuridhia kutoa chumba katika shule hiyo.

No comments

Powered by Blogger.