UZIKWASA YAANZA KUDOKEZA MTAKUWWA PANGANI


Shirika la UZIKWASA lililopo Wilayani Pangani Mkoani Tanga kupitia utekelezaji wa shughuli zake, limeanza kugusia suala la MTAKUWWA ambao ni Mpango kazi wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Katika kugusia suala hilo, Jana shirika hilo limewakutanisha pamoja wajumbe wa Kamati ya Kudhibiti Ukimwi Jinsia na Uongozi VMAC kijiji cha MEKA na Kamati ya Shule ya Msingi MEKA. Akizungumzia lengo kuu la kuwafikishia elimu hiyo wajumbe hao kuhusu MTAKUWWA, Bwana Edward Vicent Saguti afisa Jinsia kutoka shirika la Uzikwasa, amesema…. Mpango kazi huo utakaotekelezwa kwa miaka mitano nchi nzima, Bwana Saguti amezungumzia kila ambacho wanapangani wanapaswa kufanya kuhusu Mpango kazi huo. Licha ya kupata fursa ya kuuliza maswali kuhusu MTAKUWWA na kupatiwa majibu, wajumbe kwenye kikao hicho cha ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa kipindi cha miezi sita iliyopita, hawakusita kuelezea matumaini yao kuhusiana na mpango kazi huo wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto. MTAKUWWA ni Mpango kazi wa Taifa utakaotekelezwa miaka mitano kuanzia 2017/2018 hadi 2021/2022 ambapo kitaifa ulizinduliwa Jijini Dodoma, na Mpango huo uko mbioni kuzinduliwa rasmi hapa Wilayani Pangani ili uanze utekelezaji wake. Aidha kwenye kikao hicho cha ufuatiliaji na tathmini pia wajumbe hao waliwasilisha mafanikio yaliyotokana na utekelezaji wa Mpango kazi wao, pamoja na kuzimulika changamoto na vikwazo ili kuzitafutia ufumbuzi. Kutoka katika kijiji cha MEKA Khamisi Makungu Pangani fm

No comments

Powered by Blogger.