AWESO AWEKA MSISITIZO MIRADI KULETA TIJA KWA WANANCHI


Mbunge wa jimbo la pangani mheshimiwa jumaa hamidu aweso amefanya ziara ya kukakagua miradi mbali mbali ya kimaendeleo ikiwa ni harakati ya kuhakikisha miradi inayoanzishwa wilayani humo inaleta tija kwa wananchi . Akizungumza na wakazi wa kijiji cha mwera mara baada ya kukagua ujenzi wa hosteli mheshimiwa aweso amesema kuwa serikali ya wamu ya tano inaendelea kuleta miradi ya mendeleo wilayani pangani ikiwemo ujenzi wa kidato cha tano na sita, miradi ya maji ,pamoja ujenzi wa vituo vya afya katika kata ya mkalamo na mwera Aweso amesema kuwa miradi inayoanzishwa ili iweze kuleta tija katika wilaya ya pangani nivyema wazazi kuhakisha wanawekeza katika elimu na kuongeza kuwa tayari raisi ameshatuma viongozi wa wizara ya ujenzi waje kutia saini ili ujenzi wa barabara ya tanga pangani saadani uanze na zoezi hilo linatarajiwa kufanyika mapema mnamo siku ya jumatano “ndugu zangu mlisema hapa mwera mlisema kunachangamoto ya huduma ya afya kituo cha afya kimejengwa na kuna mradi mkubwa maji mkubwa utatekelezwa hapa kwa ajili ya mwera na ushongo ndugu zangu taifa lolote lilioendelea limewekeza katika elimu chonde chone tusomshe watoto wetu na na mimi nataka rais sikumoja atokee hapa pangani ‘ “Napia mheshimiwa raisi amenituma niwape salamu zenu keshokutwa siku ya jumatano tarehe 31 anatuma team ya viongozi wa wizara ya ujenzi kuja kutia saini ili ujenzi wa barabara ya tanga pangani saadani uanze nami mbunge wenu nitasimamia wafanyakazi vijana watokee pangani“ Aidha aweso akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya sokoni mjini pangani ametoa msaadawa kofia na miwani kwa watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na baiskeli za magurudumu matatu kwa walemavu wa miguu ambapo katibu wa walemavu wilayani humo bwana ibrahimu kayanda amemshukuru mbungewa jimbo hilo kwa msaada alioutoa kwa walemavu . ‘ mheshimiwa mbunge tunakushukuru sana kwa msaada huu ulioutoa kwa watu wenye ulemavu na wale wote amabao hawakufikiwa na msaada huu waleo tunaimani mheshimiwa mbunge utawafikia asante sana ‘ Na wakati huo huo katika hali ambayo haikutarajiwa aliyekuwa diwani wa kata ya pangani mashariki kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF bwana AKIDA BORAMIMI ametangaza kujiunga na chama cha mapinduzi ‘mimi akida bora mzaliwa wa pangani ambaye nilifanikiwa kumshinda ndugu Leopard Abeid katika uchaguzi wa mwaka 2015 kwa zaidi ya kura 500 lakini kwanamna ya utendandaji wangu na namna mambo ya nchi yanavyokwenda sinabudi natangaza rasmi kuhamia chama chamapinduzi ‘ Ziara ya mbunge huyo imetembelea katika shule ya sekondari bushiri kukakugua ujenzi wa nyumba za walimu ,shule ya msingi mwembeni ,jengo la ofisi za halmashuri ,maktaba ya kujisomea ,zahanati ya kikokwe pamoja na shule ya sekondari ya mwera ambapo kuna ujenzi wa hosteli kwa ajili ya kidato cha tano na sita

No comments

Powered by Blogger.