JINSI PANGANI FM ILIVYOPENDEZESHA TUZO ZA UMAHIRI WA HABARI TANZANIA


Usiku wa tarehe 29 mwezi wa 6 ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na waandishi wa Habari nchini pampja na wadau wengine wa Tasnia hiyo, kwani ulikuwa ndio kilele cha tuzo za Habari Tanzania(EJAT) tuzo zinazotolewa na Baraza la Habari nchini (MCT) tuzo zinazojumuisha waandishi wa Hbari kutoka Kila kona ya Tanzania kutoka vyombo vyote vya habari nchini ambapo mwaka huu zaidi ya kazi 600 zilishindanishwa na washindi kutangazwa katika Ukumbi wa Golden Tulip Jijini Dar es Salaam.
kituo cha Redio cha Pangani fm chini ya shirika la UZIKWASA lililopo wilayani Pangani Mkoani Tanga kilitoa washindi watatu katika vipengele mbalimbali. waandishi hao ni Mtumwa Kombora , Mwanaidi Jumanne na Rajabu Mrope.7 Mwanaidi Jummanne ndiye aliyepata ushindi mkubwa zaidi kwa kunyakua Tuzo hiyo yenye heshima kubwa katika Tasnia ya Hbari nchini huku Mtumwa Kombora pamoja na Rajabu Mrope wakipata vyeti vya ushindi pamoja na zawadi nyingine.
Mwanaidi Jumanne akiwa na Tuzo aliyoshinda EJAT 2018
Kwa mujibu wa MCT Jumla ya kazi 644 ziliwasilishwa kwa ajili ya kushindanishwa kwenye Tuzo hizi ambazo 176 (27%) kati ya hizo zimeletwa na waandishi wa habari wanawake huku zilizowasilishwa na waandishi wa habari wanaume zikiwa 468 (73%). Pangani fm imekuwa kituo pekee kutoka Mkoani Tanga kilichofanikiwa kutowa washindi katika tuzo hizo huku kikiwa moja ya vyombo vya Habari vilivyotoa wawakilishi zaidi ya mmoja katika tuzo hizo.

1 comment:

  1. Hongereni sana watu wangu. Mungu ibariki Pangani fm

    ReplyDelete

Powered by Blogger.