MADANGA WALIA NA MAJI


Wananchi wa kijijicha madanga jaira wilayani Pangani Mkoani Tanga wamelalamikia changamoto ya upatikanaji wa maji kijijini hapo na kusema kuwa wanapata maji kwa wiki mara moja. Hayo yamezungumzwa na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho ambapo wamesema kuwa wanatumia maji ya taasisi za kidini kuliko maji yanayotoka kwenye mradi wao kwasababu wasizozifahamu. “upatikanaji wa maji katika mradi wetu sio mzuri tunapata maji kupitia taasisi za kidini kuliko mradi wetu wa kijiji hii ni changamoto tunayoipata na wakati mwengine tunajiuliza kama sio hizi taasisi tungekuwa wapi sisi wananchi” Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho bwana MNYIMBONI HAMISI amesema kuwa mradi huo ulivunjwa na muheshimiwa AWESO kutokana na kutosomwa mapato na matumizi yanayoingia katika mradi huo. “kamati ya maji katika kijiji hichi haifanyi vizuri na ndio mana muheshimiwa mbunge ambaye pia ni naibu waziri wa maji JUMAA AWESO alivunja kamati ya maji na kuikabidhi mamalaka ya maji mjini pangani kutokana na kutosomwa kwa mapato na matumizi” Akijibia changamoto hiyo ya upatikanaji wa maji katika kijiji cha Madanga muhandisi wa maji wilaya bwana NOVAS WILSON amesema taarifa ya changamoto hiyo haijamfikia na kuwataka wannachi hao kutoa taarifa mapema kunapotokea changamoto ili tatizo liweze kushuhulikiwa. “ pindi kunapotokea changamoto yoyote katika mradi ni lazima taarifa zitufikie na endapo kamati wanataka kuboresha mradi wa maji pia taarifa zifike ofisini ili sisi tujuwe ni kwa namna gani tunatatua changamoto hiyo ili wananchi waweze kupata huduma ya maji” Kamati ya maji katika kijiji cha madanga jaira ilivunjwa na muheshimiwa mbunge baada ya utendaji mbovu na kusuasua kwa mradi huo na kukabidhiwa mamlaka ya maji pangani mjini.

No comments

Powered by Blogger.