WANAWAKE WAOMBA KUKAA DARASA MOJA NA WANAUME KWENYE ELIMU YA KISHERIA PANGANI


Kikundi cha UPENDO GROUP kinachojishughulisha na masula ya ujasiriamali kwa wanawake wilayani Pangani mkoani Tanga kimepatiwa elimu ya msaada wa kisheria juu ya masuala ya ndoa kwa lengo la kuondoa unyanyasaji unaowakumba wanawake. Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo VICTOR KISAKA mwanasheria kutoka taasisi ya TAWREC ,amsema lengo la mafunzo hayo ni kuwafanya wanawake kutambua haki zao ili kupunguza unyanyasaji wanaokunbana nao ndani ya ndoa zao.. “Wa kina mama wa kikundi cha Upendo baada ya kupokea elimu ya ndoa wameweza kueleza kwambamkatika ndoa zao nyingi kuna manyanyaso wanayofanyiwa na waume zao,sasa wameomba wakati mwengine tunapotoa mafunzo juu ya ndoa tuwashirikishe waume zao kwa sababu wao ndio waathirika wakubwa’
Kwa upande mwengine meneja wa ufatiliaji na tathmini kutoka shirika la Legal Service Facility Bwana SAID CHITUNG amesema lengo lao ni kuhakikisha msaada wa kisheria kwa jamii unafika kila sehemu na kuwataka viongozi kuwatumia wasaidizi wa kisheria hata kwenye mikutano yao ya vijiji. ‘’Msaada wa kisgeria unapatikana kila wilaya,hivyo lengo letu msaada huu ufike kila sehemu kwa kuanzia tumeanza kwenye wilaya ambapo Zaidi wilaya 3900 nchini msaada huu unafika,tunapenda pia kupitia mikutano ya kijiji aalikwe msaidizi wa kisheria aeleze haki ambazo wananchi wanataka kuzijua” TAWREC ni taasisi inayojishughulisha na msaada wa kisheria mkoani Tanga ambapo imekuwa ikisaidiana na tasisi ya msaada wa kisheria wilayani Pangani PACCOPA kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala yanyohusu haki zao,chini ya ufadhili wa shirika la Legal Service Facility.

No comments

Powered by Blogger.