Wananchi wa kijiji cha pangani mashariki wametakiwa kujitokeza kwa wingi hii leo siku ya jumapili ya tarehe 14/ 4/2019 katika shule ya msingi funguni ili kufanikisha zoezi la uchimbaji wa shimo la choo kwa ajili ya kukikamilisha choo cha wanafunzi wa shule hiyo.
Akizungumza na pangani fm radio kwa niaba ya mwenyekiti wa kijiji hicho, mwenyekiti wa kitongoji cha funguni bwana SALIMU KIRABA amesema kuwa wananchi hao ni pamoja na wajumbe wa kamati ikiwemo kamati ya BMU, kamati ya shule na kamati ya VIMC.
Ujenzi wa choo cha shule ya msingi funguni iliyopo wilayani pangani ulianza siku chache zilizopita baada ya vyoo vilivyokuwa vikitumika awali kufungwa na afisa afya wa wilaya kutokana kutokukidhi vigezo vya utumiaji.
No comments