WAFANYAKAZI WA KAZI ZA NDANI WATAKIWA KUTONYAMAZIA UKATILI


Wafanyakazi wote wa kazi za ndani Wilayani Pangani mkoani Tanga wametakiwa kutosita kutoa raarifa za matendo ya ukatili wanaokutana nao kwa mabosi wao ili kupata msaada. Hayo yamezungumzwa na afisa mtendaji wa kijiji cha Pangani Magharibi bwana ALFANI RASHIDI wakati akizungumza na Pangani Fm na kusema kuwa kama binti wa kazi kuna kitu ambacho hakimpendezi asisite kutoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa viongozi husika. Bwana HALFANI amewataka wale wanaoishi na wasichana wa kazi kuwalea katika upendo na maadili na kuwaruhusu kuingia katika nyumba za ibada ili waendelee kukua kiimani. Hayo yamejiri baada ya mkazi mmoja(jina tunalihifadhi) kijiji cha pangani magharibi wilayani pangani kumfanyia unyanyasaji mtoto wa kazi za ndani anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kumi na tano.

No comments

Powered by Blogger.