KIKUNDI CHA KIKOBA (MWAMKO) KIJIJI CHA MWEMBENI WILAYANI PANGANI CHAPATIWA MAFUNZO
Kikundi cha kikoba cha MWAMKO kilichopo katika
kijiji cha MWEMBENI wilayani PANGANI kimepokea mafunzo ya kujiendeleza kupitia
kikoba endelevu ili kupata elimu ya kujikwamua kiuchumi.
Kikundi cha mwamko kilichofikia hatamu
yakujichangisha fedha kwa ajili ya kumleta
mwalimu kutoka dar es salaam kwaajili yakuwafikishia elimu ya kikoba
endelevu pia kimewashirikisha vikundi vya vikoba kadhaa kutoka katika mbali
mbali ikiwemo madanga, boza, na
kigurusimba.
Akizungumza katika mafunzo hayo mratibu wa vicoba endelevu
kutoka taasisi ya buta sastenable
development agensi jijini dar es salaam bwana ANDREA MBWAMBO amesema kuwa lengo la vicoba
endelevu ni kila mwananchi na kila mtanzania kuwa na maisha bora kupitia vicoba
endelevu na wameona kuanza na wilaya ya pangani kwa sababu wameona wanauhitaji
na pia lengo ni kuisambaza elimu hiyo kwa maeneo mengine.
‘’lengo letu kubwa la vicoba endelevu ni kila
mwananchi kila mtanzania kuwa na maisha bora kupitia vicoba endelevu sasa
tulipanga program yakutoa mafunzo kwa nchi nzima lakini tumeona kuanza na
wilaya ya pangani kwa kuwa tumeona wana uhitaji na wameona umuhimu wake kwa
hiyo ninachowataka waendeleze hii elimu na hatuishiii hapa bali tutaisambaza
sehemu mbali mbali’’ amesema Mbwambo.
Amewataka wakazi wa kijiji cha mwembeni na wote
waliopata mafunzo hayo kuhakikisha wanaisambaza kwa wengine na kusema kuwa watu
wengi wamekosa elimu hiyo ya vicoba endelevu jambo linalowanyima fursa ya
kufikia maendeleo.
‘’kwa
ujumla tumefurahi kuwaona na tumefurahi kukutana na wakazi wa pangani pia
wametupokea vizuri na hata darasa tulilolitoa wamelifurahia watu wengi wamekosa
hii elimu tuliyoitoa kwao ni kama tunu na ninachowaomba hii elimu ya vicoba
endelevu waifikishe kwa wananchi wengine ambao leo hawakuhudhuria’’ amesema Mbwambo.
Bwana ally semfuko ni afisa mtendaji wa kata ya
madanga na pia alikuwa mgeni rasmi wa mafunzo hayo kwa upande wake amekitaja
kijiji cha mwembeni kuwa cha mfano wa kuigwa kutokana na kujitolea hasa katika
masuala ya kimaendeleo.
‘’maagizo mengi yanayopelekwa katika vijiji kijiji
cha mwembeni kinachukuwa nafasi kubwa ya kutekeleza, ninachowaomba wana
mwembeni shughuli zinazofanyika hapa zinamuelekeo na zinaridhisha, tumepata
mwalimu wakuja kutuelekeza hivyo basi nawaomba mafunzo haya yalete mabadiliko’’
amesema Semfuko.
Kwa upande wao wajumbe walioudhuria mafunzo hayo
wamesema kuwa wamepata elimu ya kutosha ambayo itawafanya kufikia malengo yao,
na kuwataka vijana, wakinamama kujitokeza kwa wingi katika kujiunga na vikundi
vya kicoba endelevu ili kupata mafanikio.
‘’kwa sababu ni mara yangu ya kwanza kupata elimu
hii, mimi nashukuru nimepokea vizuri na yamenipa mwanga wakusonga mbele
ninachowaomba wakinamama na vijana tuunde vikundi ambavyo vitatuweka pamoja
katika kujikwamua kiuchumi’’ mmoja kati ya wajumbe.
No comments