MADAKTARI PANGANI WAZUNGUMZIA HATARI YA UGONJWA WA U.T.I
Ugonjwa wa njia ya haja ndogo kwa maana ya U.T.I Wilayani Pangani unatajwa kuwa
miongoni mwa magonjwa sugu kumi yanayowatesa watu wengi kwenye jamii,
ikifuatiwa na Magonjwa ya njia za hewa.
Akizungumza katika kipindi cha ASUBUHI YA LEO
kinachorushwa na kituo hiki, Mtaalamu wa masuala ya kinamama katika hospitali
ya wilaya ya Pangani Daktari KOMBO MUHINA amesema kuwa miongoni mwa Magonjwa hayo
yanayosumbua Wilayani humo Ugonjwa wa U.T.I unashika nafasi ya Pili ukiongozwa
na magonjwa ya Njia za hewa.
“Katika magonjwa kumi yanayosumbua Pangani, ugonjwa
wa njia za Mkojo unashika nafasi ya pili katika hospitali yetu na katika wilaya
yetu ya Pangani, ndio maana tumeona ni vizuri kulizungumza ili wananchi waweze
kuelewa. Linaloongoza ni magongwa ya njia za hewa, hili ndio tatizo kubwa la
kwanza likifuatiwa na hili la njia ya mkojo” Amesema Daktari Kombo Muhin.
“Kimsingi tatizo kubwa sana, sehemu nyingi ambazo
tumezunguka hapa Tanzania utalikuta katika hospitali linakuwa ni tatizo namba moja
au namba mbili, kwa sababu gani, watu hawa tunawatibu lakini wakitoka wanarudi
katika yaleyale mazingira ambayo ni hatarishi, lakini kingine kuongezea hapa
ambalo pia ni onyo vilevile kwa wakazi wa Pangani na sehemu zingine ni kwamba
inabidi usitumie dawa yoyote pasipo kuandikiwa na daktari” wamesema Madaktari
hao kutoka Muhimbili na kuongeza kuwa…….
Ili kufanikiwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo
madaktari hao wameshauri wananchi kufika mapema katika vituo vya kutolea huduma
za Afya, pamoja na kushauri jamii kujali usafi kuanzia wa mwili na mazingira
wanayoishi.
“Baada ya
matibabu mtu anatakiwa azingatie kutumia maji mengi, usafi wake wa mwili lakini
pia usafi na watu wale wanaomzunguka ili ugonjwa usiwe kwake tatizo na kwa
jamii pia ambayo inakuwa inamzunguka, wakifanya hayo tatizo hili litashuka
chini” Wakiongea kwa msisitizo wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili
Jijini Dar es Salaam.
Kadhalika Dalili za ugonjwa huo zinaweza kuwa kusikia maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo, homa na maumivu katika viungo vya mkojo, kuhisi kuhitaji kujisaidia haja ndogo mara kwa mara na pia haja ndogo kuwa na hali ya kuunguza wakati wa kujisaidia.
No comments