Mwenge wa uhuru unatarajiwa kufika wilayani pangani mkoani tanga na kukimbizwa katika viunga vyake Tarehe 6 mwezi huu wa 7 ukienda sambamba na kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo wailayani humo.
Hayo yamezungumzwa na Bwana Isaya Mbeje ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri wa wilaya ya Pangani wakati akifanya mahojiano maalaum na Pangani Fm kuhusiana na ujio wa mwenge wa uhuru,Ambapo amesema kuwa Mwenge wa uhuru unatarajiwa kufika wilayani pangani Tarehe 6 mwezi huu ukitokea katika wilaya ya Muheza na kupokelewa kwenye kijiji cha Masaika akibainisha kuwa
“maandalizi ya kufika kwa mwenge huu wa uhuru yanaendelea vizuri kama halmashauri tumejipanga kuanzia mapokezi siku ya tarehe 6 jumamosi hii katika shule ya msingi masaika majira ya saa 2 kamili asubuhi pamoja na ujumbe wa mwenge huo tukitarajia pia kutakuwa na shamrashamra mbali mbali pamoja na mkesha ”,Alisema bwana Issaya
Bwana Isaya ameongeza kuwa mapokezi hayo yataambatana na shamrashamra mbali pamoja na mkesha ambao utafanyika katika shule ya msingi masaika huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kwenda kuulaki mwenge huo,
”baada ya kupokea mwenge katika kijiji hiko cha masaika kutakuwa na mkesha wa awali,katika mkesha huu kutwakuwa na burudani mbali mbali hivyo basi kama halmashauru tunawaomba wananchi wa vijiji vyote vinavyoizunguka masaika wafike Ikiwemo Kimang”a madanga hata bushiri kufika bila ya kukosa” Aliongeza bwana Isaya
Aidha amemalizia kwa kusema kuwa mwenge wa uhuru utapita katika miradi kwa ajili ya kuzindua ikiwemo Zahati ya kijiji cha Madanga ambayo inahistoria pana kutokana na zahati hiyo kuwekewa jiwe la msingi na Baba wa Taifa Mwalim julias Kambarage Nyerere 1965.
“Mwenge huu pia utakuwa na fursa kufungua miradi mbali mbali wilayani kwetu,tutakwenda shule ya sekondari ya wasichana macapchini mivumoni ambapo mwenge utazindua clab ya wanafunzi ya kupambana na rushwa sambamba na kukagua kitalu cha mipopoo baada ya hapo mwenge utaelekea madanga ambapo utafika katika jingo la zahati ya kijiji cha madanga ambayo inahistoria ya ndefu ya kuwekewa jiwe na mwalim julias Kambarage Nyerere”
Mwenge wa uhuru utakesha katika viwanja vya Pangani Magharibi ambapo kutakuwa na Maonyesho mbali mbali sambamba na burudani,Huku mbio hizo za mwenge kwa mwaka huu zikibeba kauli mbiu isemayo Maji ni Haki ya Kila Mtu, Tutunze Vyanzo Vyake na Tukumbuke Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
No comments