MWENGE WAZIWAKIA RUSHWA PANGANI


Jamii wilayani Pangani mkoani Tanga imetakiwa kushiriki kikamilifu katika kupiga vita vitendo vya rushwa nchini ili kusaidia taifa kupiga hatua katika masuala ya kimaendeleo. Hayo yamezungumzwa na Kiongozi wa Mbio za mwenge kitaifa mwaka huu 2019 ndugu MZEE MKONGEA ALLY wakati wa akizindua klabu ya kupinga rushwa inayoundwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya masista wa ivumoni ambapo amesema mapambano ya rushwa ni ya jamii yote. “Suala la ni tatizo sugu katika taifa letu, tushirikianae kwa pamoja mapambano ya rushwa siyo ya serikali pekee yake,lakini inaanza na mimi na wewe, kwa sasa ikibainika unajihusisha na masuala ya rushwa kifungo ni miaka ishirini au thelathini jela, lakini siyo hilo tu hawa mafisadi wahujumu uchumi wala rushwa wameanzishiwa mahakama yao maalumu ambayo imeanza kufanya kazi rasmi mwaka 2016 kesi zipatazo 1340 zimefikishwa mahakamani na watuhumiwa wapatao 685 wamehukumiwa katika magereza mbalimbali” alisema Ndugu mkongea. Sambamba na hayo Ndugu Mzee amewataka wakinababa kuacha kuwadhalilisha na kuwanyanyasa kinamama huku akimuagiza mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Pangani kuchukua hatua kali dhidi ya watakaobainika kufanya vitendo hivyo. “Na nitoe onyo kwa wakinababa wanaume wenzangu tumekuwa na tabia mbaya ya kuwatelekeza wakinamama, tabia hii ni tabia mbaya sana inarudisha nyuma kwa sababu sisi tumezaliwa na wakinamama , hivyo OCD tunaelewa katika jeshi la polisi kuna dawati, zinapokuja kesi kama hizi za kuwadhalilisha wakinamama na watoto, kesi hizi zisiishie kifamilia wote watakaojikita na makosa haya basi wachukuliwe hatua kali za kisheria” ameongeza Ndugu Mkongea. Hayo yamejiri katika mbio za mwenge kitaifa katika wilaya ya Pangani ambao umezindua mradi mmoja kukagua miradi mitatu kuweka mawe ya msingi katika Miradi miwili huku mradi mmoja ukikataliwa kuzinduliwa kutokana na kukosekaka kwa vipimo vya bomba. Mbio za mwenge mwaka huu 2019 umebeba ujumbe usemayo Maji ni haki ya kila mtu tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

No comments

Powered by Blogger.