Baadhi ya watumishi kutoka idara ya afya na elimu wilayani Pangani mkoani Tanga wametoa shukrani zao kwa shirika la UZIKWASA lililopo wilayani humo kufuatia mafunzo ya kijitathimini utandaji wao ili kufanya kazi itakayokuwa na tija Zaidi kwa jamii.
Hayo yamesemwa katika siku ya kwanza ya mafunzo ambapo watumishi hao wamesema wamefahamu nafasi zao katika ngazi mbalimbali za kiuongozi na kusikiliza katika ngazi tatu za,pamoja na aina za ukatili.
Mimi nashukuru kuhudhuria mafunzo haya kwa sababu nimejifunza kwamba mimi ni kiongozi kuanzia ngazi ya family na sehemu ambayo nafanyia kazi,mimi nimejifunza vingi kwanza ngazi tatu za kusikiliza ambazo ni KICHWA,MOYO NA HATUA,mimi pia kwa upande wangu nimejifunza aina za sauti na namna ya kuheshimu sauti hata ndogo kiutendaji.
Kwa upande wake muwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA, JOSEPH PENIEL amesema mbali na kuwepo kwa miundombinu mbalimbali ya kushuhghulikia ukatili katika jamii kitu kinachohitajika ni kujifanyia tathmini wenyewe kuona namna gani zinashuhghulikia matukio ya ukatili.
Kuna mahakama,kuna hospitali kuna shule hizo ni structure muhimu sana katika kushughulikia ukatili lakini bila kujimulika wenyewe ukatili hauwezi kuisha .
Hayo yamejiri katika mafunzo yenye lengo la kuwezeshana kama viongozi ngazi ya wilaya kutumia mbinu wezeshi katika utendaji kutambua na kushuhghulikia vyanzo vya ukatili na mahitaji yao kiutendaji ili kuboresha mahusiano yao wale wanao waongoza.
No comments