Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa kushirikiana na shirika la UZIKWASA wamezindua Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wilayani Pangani.
Hata hivyo Katika kipindi cha miezi miwili shirika la UZIKWASA kupitia Redio yake 107.7 Pangani FM tayari ilishaanzisha mijadala miongoni mwa jamii juu ya MTAKUWWA. Pia kwa kupitia matangazo ya moja kwa moja kwa njia ya mtandao, ukurasa wake wa facebook https://www.facebook.com/panganifm107.7 pamoja na Blog yake.
uzinduzi wa MTAKUWWA wilayani Pangani uliambatana na Tamasha la ugawaji tuzo kwa vijiji bora katika mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto wilayani humo, tukio lililokutaniasha wananchi, viongozi mbalimbali wa kiserikalipamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya kijamii huku mgeni rasmi akiwa katibu tawala wa wilaya ya Pangani Bwana Mwalimu Hasani Nyange ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Zainab Abdallah
No comments