Kijiji cha Kimang’a kilichopo wilayani Pangani Mkoani Tanga kimeibuka kidedea katika mashindao ya vijiji bora kwenye mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto wilayani Pangani.
Hayo yamejiri katika Tamasha la Ugawaji Tuzo kwa Vijiji Bora katika Mapambano dhidi ya Ukatili wa Wanawake na Watoto Wilayani Pangani lililofanyika tarehe 15 mwezi wa 6 mwaka huu wilayani Pangani Mkoani Tanga.
Mashindano hayo hufanyika kila mwaka ambapo awali yalikua yakihusisha kamati za Vmac na kamati za shule.
Pamoja na kupewa tuzo pia kijiji hicho kilizawadiwa hundi ya shilingi laki nane kama washindi wa kwanza.
Katika siku hiyo viongozi wa vijiji wamezungumzia mafanikio yao na kuelezea umma namna gani wameweza kufanikiwa kuleta mabadiliko chanya katika kupambana na ukatili wa kijinsia vijijini kwao.
No comments