PANGANI FM YANG'ARA TUZO ZA HABARI NCHINI


Jumla ya waandishi 3 wa Kituo cha Pangani fm redio chini ya shirika la UZIKWASA wameteuliwa kushiriki tuzo za umahiri na uandishi wa habari zinazoandaliwa na Baraza la Habari nchini Tanzania M C T. Akitangaza majina hayo kupitia ukurasa rasmi wa Facebook Baraza la Habari nchini MCT , katibu mtendaji wa baraza hilo Kajubi Mukajanga amewataja Rajabu Mrope,Mtumwa Kombora,na Mwanaidi Jumanne huku akiwataka waandishi ambao hawakutajwa msimu huu wasubiri mwakani bila kukata tamaa. Baraza la Habari nchini limekuwa na utaratibu wa kuaandaa tuzo za umahiri wa uandishi wa habari kwa wanahabari nchini Tanzania ambapo tuzo hizo zitatolewa June 29,wiki hii jijini Dar Es Salaam. Kinyang’anyiro hicho kigumu hujuimuisha kaz za waandishi wa habari kutoka mikoa yote nchini katika vyombo vya habari vya aina mbali mbali, ambapo mwaka huu jumla ya kazi 644 zimewasilishwa katika mchuano huo.

No comments

Powered by Blogger.