Serikali Wilayani Pangani mkoani Tanga imesema mpango wa kupokea wanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari Mwera iliyopo Wilayani humo upo pale pale na wanataraji kupokea wanafunzi wa chaguo la pili yaani Second Selection
Hayo yamezungumzwa na Katibu Tawala Wilayani humo Mwalimu Hasan Nyange wakati wa mahojiano maalum na kituo hiki ambapo amesema kwa sasa afisa elimu sekondari yupo mkoani Dodoma kwaajili ya ufuatiliaji wa kibali na wanatarajia kupata wanafunzi baada ya kukamilisha taratibu za kupata kibali
“
Tunavyozungumza sasahivi asifa elimu sekondari yupo Dodoma kunataarifa ndogo ambayo imetakiwa tunaamina baada ya kupokelewa taarifa hiyo atapata kibali tukishapata kibali tutakuwa miongoni mwa shule sita ambavyo tutapata wanafunzi waliochaguliwa second selection”amesema Mwalimu Nyange
Aidha BW NYANGE amesema baada ya kufanyika ukaguzi shule hiyo ilionekana mapungufu yaliyokwamisha kuanza kupokea wanafunzi hivyo wao kama viongozi wakahakikisha mapungufu yamefanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma ya umeme na maji inapatikana ili kuweka mazingira wenzeshi ya kimasomo kwa wanafunzi watakaochaguliwa.
“
Baada ya tume ya uchunguzi kutoa ripoti ya iliyonesha mapungufu katika shule ile sisi kama viongozi tulipambana ili kuhakikisha kuwa yale mapungufu tunayafanyia kazi”amesema Mwalimu Nyange.
“Tulihakikisha tunapata huduma ya maji kwa kuchimba kisima ,tulihakikisha huduma ya umeme inapatikana na tumefanikiwa kwani umeme umeanza kuwaka july 28” amesema Mwalimu Nyange.
“Tayari tumekwisha ingiza vitanda mabwenini,mabweni yamepakwa rangi ,tulikuwa tutumie madarasa ya awali na tunavyozungumza sasahivi madarasa matatu yameshajengwa yameshapigwa pati na fundi ameniahidi ikifika tarehe 5 mwezi huu anakabidhi madarasa takiwa yamekamilika, amesema mwalimu Nyange
Zaidi ya kiasi cha shilingi Milioni 40 zilimechangwa na wadau wa Elimu na wananchi mbalimbali wa Wilaya ya Pangani baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kuongoza harambee wakati wa kongamano la wadau wa Elimu Wilayani humo kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wasichana wa kidato cha tano na sita katika shule Sekondari Mwera mkoani Tanga mwezi oktoba mwaka 2018.
No comments