HALMASHAURI YA WILAYA PANGANI KUTATHMINI JUU YA MATUMIZI YA B.M.U


Halmshauri ya wilaya ya Pangani imesema inafanya tathimini ili kuona kama kuna uwezekano wa kuendelea kutumia B M U katika ukusanyaji wa mapato kama hapo aewali au kutumia watumishi wa halmashauri hiyo kama wafanyavyo sasa lengo likiwa ni kupata mapato ya kuridhisha. Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Pangani Bwana ISAYA MBENJE wakati akizungumza na kituo hiki ambapo amesema watafanya tathimini baina ya B M U na watumishi wa halmshauri kujua ni nani walifanikiwa zaidi na ndipo watakapoamua nani awe mkusanyaji wa mapato ya halmashauri. “Tunaendelea kufanya tathimini pale tulipokuwa tunatumia BM U tulifnikiwa kiasi gani,na sasa tunatumia wataalamu wetu je kuna changamoto gani? Nini changamoto ya kutumia mawakala au kutumia watumishi baada ya hapo tutafanya majumuisho,lakini hili ni kuangalia miongozo ya serikali inatekelezwa kuongeza wingi wa ukusanyaji wa mapato ya halmshauri” Bwana MBENJE ameongeza kuwa kuwa mabadiliko yakijua mara baada ya taarifa ya serikali ambayo ilisema umakini umepungua katika ukusanyaji wa mapato ikiwemo mapato ya halmashauri na ndipo walipoona haja ya kutumia watumishi wa serikali kwa sasa. Kuna wakati halmashauri zilikuwa zinatumia mawakala kukusanya mapato ndipo halmashauri ya wilaya ya Pangani ilikuwa inatumia B M U kukusanya mapato lakini baadae srikali inaona hakuna umakini katika ukusanyaji wa mapato na ndipo tukaona tuanze kutumia watumishi wetu na tukaona B M U tuwasitishe kukusanya. Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura ya 290, ilizizipa uwezo Mamlaka za Serikali hizo kutoza na kukusanya kodi, ushuru na ada mbalimbali kama vyanzo vya mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa,kabla ya sharia ya fedha iliyopita kuelekeza kuacha kutumia mawakala kutokana na kugundua kushuka kwa umakini katika ukusanyaji wa mapato hususani kwa halmshauri mbalimbali hapa nchini.

No comments

Powered by Blogger.