HUU HAPA UFAFANUZI WA UWEPO WA SERIKALI ZA VIJIJI KATIKA MAKAO MAKUU YA WILAYA PANGANI


Halmashauri ya wilaya ya Pangani imetolea ufafanuzi juu ya uwepo wa serikali za vijiji katika makao makuu ya wilaya mjini Pangani tofauti na serikali za mitaa kama maeneo mengine nchini. Akizungumza na Pangani fm mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani ISAYA MBENJE amesema makao makuu ya wilaya kwa sasa yanajumuisha mamlaka za vijiji na mji huku pia matumizi ya sheria za mipango miji zote zinaendelea kutumika hivyo majukumu ya utekelezaji wa shuhghuli za serikali hutegemeana na suala husika. “Hapa makao ya wilaya ni mjini,lakini ni mjini na pia kuna vijiji ambavyo bado havijafutwa,kwa hiyo kuna sharia na 4 na 5 baado zinatumika kwa pamoja na hapa suala ni kuelewa mipaka tu ya kazi”. Akitolea mfano wa masuala ya umiliki wa ardhi hususani katika suala la ugawaji wa viwanja Bwana MBENJE amesema serikali ya kijiji katika hilo itahusika katika eneo ambalo halijapangwa kwa mujibu wa sharia za mipango miji. 'Halamshauri ya kijiji inaweza kugawa kiwanja kwenye eneo ambalo halijapimwa,lakini eneo likishapimwa na kusajiliwa kwa msajili wa mipango miji maana yake hapo kijiji hakiwezi kuhusika kwenye hilo,vijiji vitaendelea kutoa hati yake zake kimila kwa mujibu wa utaratibu uliolezwa kwenye sharia ya ardhi ya vijiji” Pangani mashariki na pangani magharibi ni vijiji ambavyo vipo katika makao ya wilaya ambapo ni mjini na ili kuwa na hadhi ya mji mdogo kila kijiji kinatakiwa kuwa na vigezo vifuatavyo,Kuwe idadi ya watu wasiopungua elfu kumi (10,000),Kuwe na huduma za jamii zifuatazo: Shule ya Sekondari, Kituo cha Afyana Mahakama ya Mwanzo,Kuwe na

No comments

Powered by Blogger.