VMAC KIJIJI CHA LANGONI WATOA MAHINDI KWA AJILI YA CHAKULA SHULENI
Kamati ya kudhibiti UKIMWI jinsia na Uongozi VMAC
kijiji cha Langoni wilayani Pangani leo wametoa msaada wa mahindi Kilo mia tatu
pamoja na Pesa taslimu shilingi elfu thelathini katika shule ya msingi ya
kijiji hicho kwa ajili ya kufanikisha upatikanaji wa chakula shuleni hapo.
Akizungumza wakati wa zoezi la Utoaji wa Msaada huo
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi IMANI BAKILI amesema kuwa wameamua kutoa msaada
huo kutokana na kuwawezesha wanafunzi wa shule hiyo kupata chakula wakiwa
shuleni ili kusaidia uwelewa mzuri wa masomo kwa wanafunzi hao.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Langoni Mwalimu MOHAMEDI SALUM ameishukuru kamati hiyo kwa kutoa msaada huo
kwani utasaidia kutatua changamoto ya chakula kwa wanafunzi pamoja na kambi ya wanafunzi wa darasa la
saba wanaojiandaa kufanya mtihani.
Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wameelezea kufurahishwa na
msaada huo wa mahindi uliotolewa na kamati hiyo kwani itasaidia, kwa kuwa kuna baadhi
wanafunzi wenzao ambao hutembea umbali mrefu hadi kufika nyumbani wakiwa na
njaa.
Hii inajumuisha shughuli mbalimbali za kujitolea
zilizofanywa na Kamati hiyo ya VIMAC ya kijiji cha Langoni ndani ya mwaka huu
ambapo hivi karibuni walijitolea kuchimba msingi wa kupitishia mipira ya maji
katika kijiji chao.
No comments