KAMATI YA VMAC KIJIJI CHA MKWAJUNI YATOA MSAADA KWA WAGONJWA WA HOSPITALI WILAYANI PANGANI
Kamati ya Kudhibiti Ukimwi Jinsia na Uongozi VMAC ya
Kijiji cha Mkwajuni imefanya ziara ya kutembelea wagonjwa waliolazwa katika
Hospitali ya Wilaya ya Pangani, kwa ajili ya kutoa msaada na kuwapa pole ikiwa
ni utekelezaji wa mikakati yao kwa mwaka 2017.
Wakizungumza baada ya kukamilisha zoezi hilo Baadhi
ya wawakilishi wa kamati hiyo Bi Judi Luka ambaye ni mjumbe na Bi Fatuma Mnyamisi
Muhaka Afisa Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Mkwajuni, wamesema kuwa kufikia hatua
hiyo ni faraja kwao kwani kwa muda mrefu walitamani kukamilisha ajenda hiyo,
kama mpango uliotakiwa kukamilika ndani ya mwaka huu 2017.
‘’Nashukuru mungu kwa siku nyingi tulikuwa
tunapigania kutoa msaada kwa wagonjwa wa hospitali lakini leo tumetekeleza, na
tumegawa kama tulivyotarajia.’’ Mmoja wa wajumbe.
Awali wakipokea msaada huo baadhi ya wagonjwa
waliopata nafasi ya kupaza sauti zao, pamoja na kuzielekeza shukrani zao kwa
wanakamati hao, wahudumu wa afya na madaktari, wamesema utaratibu huo ambao
jamii imejiwekea wa kuwatembelea mara kwa mara hakika inapendeza.
‘’Nilikuwa
nasumbuliwa na tumbo lakini baada ya vipimo nimeonekana nina apendex, kwa kweli
inapendeza kupata msaada huu, ninachowaombea kwa mungu awape moyo huu huu.’’
Amesema mgonjwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Mkwajuni Bi
Rehema Kasimu amesema kuwa pamoja na kwamba hii ni mara yao ya kwanza, zoezi
hilo litakuwa endelevu kwao huku akiwaomba wanakamati wengine kuguswa na maeneo
kama magereza, hospitali na kadhalka.
‘’Nilipanga
kuwapatia wagonjwa msaada wa sabuni na mpira kwa vijana kwa ajili ya burudani
za michezo na tutawapatia leo, ninachoomba kamati nyingine kuwapatia wagonjwa
msaada ili tuwape moyo, na kwa kamati yetu ya mkwajuni hii ni mara yetu ya
kwanza na munmgu akipenda itakuwa ni endelevu’’ mwenyekiti wa kamati.
Naye Muhudumu wa afya katika hospitali hiyo
aliyewaongoza wanakamati hao kwa kuwatembeza kila WODI Bi Mariam Ally, amesema
kuwa zoezi hilo liwefunza kwa wengine kwani linaongeza upendo na faraja kwa
wagonjwa.
No comments