YALIYOJIRI KWENYE KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WILAYANI PANGANI
Uhamasishaji
wananchi katika kuchangia ujenzi wa kitua cha afya cha Mwera wilayani Pangani umesitishwa
hadi pale wataalam wanaosimamia ujenzi huo watakapokabidhi mpango kazi wa
ujenzi wa kituo hicho.
Suala hilo limeibuka
wakati wa kikao cha Madiwani wilayani Pangani kilichofanyika hivi karibuni
ambapo limezua vuta ni kuvute kwa baadhi ya madiwani walipokuwa kwenye kikao hicho
hali iliyosababisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mheshimiwa
SEIF ALLY kutumia sheria ya kupigia kura kwa ajili ya maamuzi ya kuhamasisha au kutokuhamasisha wananchi
kuchangia ujenzi huo ambapo baada ya kupiga kura waheshimiwa madiwani kwa
pamoja wameamua kusubiri mpango kazi huo
yaani BOQ kutoka kwa wataalam.
“Wanao sema
twendeni kwa wananchi tukaanze
kuwaelemisha leo, alafu BOQ itafuata baadae kama maelezo ya utetezi ya katibu wangu
alivyosema kwamba tuacheni na shughuli zimeshaanza kufanyika, sawa? wanyooshe mikono juu, haya kura tano hizo.
Haya wanaosema mpaka tupate BOQ ndio twende kwa wananchi kura kumi hizo kwahiyo
mchakato huu tunausimamisha mbaka tupate BOQ. Amesema Mheshimiwa Seif.
Hayo yameibuka
baada ya diwani wa kata ya Mwera Mheshimiwa JAMHURI
GOGO kuwaomba viongozi wa kata nyingine kuchangia ujenzi wa kituo hicho ambacho
kitawasaidia wananchi wa maeneo tofauti hasa kuanzia aneo la Bweni hadi Mkalamo.
“Kituo cha
afya cha Mwera, sasa kinataka kiboreshwe zaidi kwa nia nzuri tu kwa maslahi
mapana ya wana Pangani, wanafanyaje sasa katika kutoa msaada hususani katika
michango mbalimbali yaani jambo lolote ambalo litaonekana lina maslahi kwa wanapangani
hususani katika kujenga kituo chetu cha afya kile kinatugusa sisi.” Alisema
Mheshimiwa Gogo.
Katika kutoa
ufafanuzi juu ya suala hilo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Bwana SABAS
DAMIAN CHAMBASI amesema kilichoelezwa na
diwani Gogo ni jitihada za halmashauri na vijiji kwani serikali kuu tayari imekwishatoa
shilingi milioni 400 za ujenzi wa kituo hicho.
“Fedha
zililetwa milioni mia nne na serikali kuu na hiyo ni sehemu ya jitihadi
zinazotakiwa kuchangia maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya, sasa mpango wetu
kama anavyoeeleza Mheshimiwa diwani wa kata ya Mwera kwamba sasa anataka
mchango wa jitihada kutoka halmashauri , kutoka kwenye vijiji na kwa watu
binafsi.” Amesema Bwana Sabas.
Pamoja na
hayo aliyekuwa diwani mteule wa kata ya Madanga Bwana ATHUMANI TUNUTU kupitia chama cha
mapinduzi CCM ameapishwa kuwa diwani rasmi wa kata hiyo na kukabidhiwa vitendea kazi ili kuanza kuwatumikia
wananchi wa kata hiyo baada ya kumalizika kwa uchaguzi mdogo uliofanyika Februali 17 mwaka
huu.
No comments