VMAC YA KIJIJI CHA MWEMBENI YATOA MSAADA WA VIFAA VYA HUDUMA YA KWANZA MASHULENI
Kamati ya kudhibiti Ukimwi Jinsia na Uongozi ya
kijiji cha MWEMBENI leo imetoa msaada wa vifaa vya Huduma ya Kwanza katika shule
za Sekondari ya Bushiri na Boza pamoja na shule za msingi Mwembeni na Madanga
ikiwa ni mchango wao katika kuendeleza gurudumu la elimu.
Akizungumza na Pangani fm mwenyekiti wa kamati hiyo
Bi PILI YUSUFU amesema kuwa lengo la
kutoa msaada huo wa chakula pamoja na vifaa vya huduma ya kwanza ni kusaidia upatikanaji
wa chakula katika shule hizo na kusaidia utolewaji wa huduma ya kwanza endapo
mwanafunzi atapata ajali.
Kwa upande wa walimu wa shule hizo zilizopata msaada
wa chakula na vifaa hivyo wameishukuru sana kamati hiyo kwa mchango wao
wakielezea kwamba utawasaidia kwa kiasi kikubwa kwani umefika kwa wakati
muafaka.
Kamati hiyo pia imetoa mahindi kilogram 100, Mchele
kilogram 30 vifaa vya huduma ya Kwanza kwa shule ya msingi Mwembeni, Mahindi
gunia 1 na vifaa vya huduma ya Kwanza kwa shule ya sekondari bushiri huku shule
ya Msingi Madanga na Sekondari Boza zikipatiwa vifaa vya huduma ya kwanza
pekee.
No comments