PANGANI YAZIDI KUAMKA, KIWANDA CHA KUCHATAKA NYUZI ZA MAKUMBI CHAANZA KAZI
Hatimae kiwanda cha
utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na
nyuzi za makumbi ya nazi wilayani Pangani umeanza huku kiwanda hicho kikipewa jina la Pangani Coconut Fibre .
Pangani Fm imetembelea eneo la kiwanda hicho kilichopo eneo la Funguni na kuzungumza na msimamizi mkuu wa shughuli za uzalishaji Bwana Salim Aziz
Suleiman na kusema kuwa shughuli za uchakatakaji wa makumbi ulisimama kutokana na kuhangaikia masuala ya masoko za bidhaa watakazozalisha.
‘’Kwa kipindi cha mwanzo hatukupata
soko kwa kuwa mwanzo siku zote ni mgumu na uwezi ukatengeneza bidhaa bila ya
kujuwa utazipeleka wapi, lakini kwa sasa tunashukuru tumepata watu watakao
zinunua, tunatengeneza bidhaa nyingi kama mbolea, kamba, magororo na mikoba na
siku zinavyozidi kwenda tutakuwa tunatengeneza bidhaa zinazotokana na haya
material’’ amesema Salim
Baadhi ya
wafanyakazi kiwandani hapo wameelezea namna ambavyo shughuli zinazoendeshwa
zitakavyosaidia kuondoa sakata la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana wilayani
Pangani.
‘’kiufupi kutokana na wilaya yetu ya pangani
hajira ni chache, tumeona tuchangamkie hii fursa ili tuweze kuwajibika katika
kazi hizi za makumbi, tunamshukuru sana muajiri wetu Aziz na tunafanya kazi
kwa moyo mmoja’’ alisema mmoja wa wafanyakazi kiwandani hapo.
Hayo ndio maajabu ya mti wa mnazi ambapo kutokana na makumbi bidhaa mbalimbali
zinatarajiwa kuzalishwa hapa ikiwemo Magodoro, Mabusati, Kamba, Mbolea, Mapambo
mbalimbali ya majumbani na ofisini huku matarajio yao ni kuajiri vijana wengi
zaidi kutegemeana na soko litavyokuwa kubwa, ukizingatia Tanzania inelekea
katika uchumi wa viwanda.
No comments