WAKULIMA PANGANI WAHIMIZWA KUANDAA MASHAMBA
Wakulima Wilayani Pangani wametakiwa kuongeza kasi
ya utayarishaji wa mashamba ili kuendana na msimu wa mvua zinazotarajiwa
kunyesha hivi karibuni.
Hayo yamezungumzwa na afisa kilimo wilayani Pangani Bwana
Ramadhani Zuberi wakati wa mahojiano maalumu kupitia kipindi cha Makutano kinachorushwa
na Pangani Fm na kusema kuwa kasi ya
utayarishaji mashamba ni ndogo na kuwataka wakulima kujiandaa ili kuendana na
msimu wa mvua.
‘’Kama wakulima wanavyojua na kwa wale wakulima wageni
ni kwamba mwezi huu ni wa mwisho kwenye kutayarisha mashamba lakini nikiangalia
kasi kule mashambani ni ndogo na sasa tuna wiki moja ya kufanya kazi hii ya kulima
kwa sababu juzi tulikuwa kwenye kikao cha hali ya hewa na jana naona mkurugenzi
katoa pia taarifa za muelekeo wa hali ya hewa ni kwamba kwa mkoa wetu wa Tanga tunatarajia
kupata mvua za wastani’’amesema Afisa Kilimo
Maeongeza kuwa kuna baadhi ya mazao ambayo yanatakiwa
kupandwa mwanzoni mwa msimu kabla ya mvua ili yaweze kuyalimwa mara mbili kwa
mwaka na kuwataka wananchi kuhamasishana katika masuala ya kilimo.
No comments