WAVUVI PANGANI WATAKIWA KUFUATA SHERIA
Wavuvi Wilayani Pangani Mkoani Tanga wametakiwa
kufuata sheria za uvuvi na endapo sheria hizo si rafiki kwao ni vyema kujenga
hoja ili zifanyiwe marekebisho.
Hayo yanajiri kufuatia malalamiko ya wavuvi juu ya
kile walichokiita kuwa kwa sasa wanahali ngumu ya maisha baada ya kutakiwa kutumia nyavu za uvuvi za jicho la milimita 10
kwani hapo awali walikuwa wakitumia nyavu za jicho la milimita 8 kuvulia dagaa
jambo ambalo linatajwa kuwa kinyume cha sheria.
Akizungumza katika kikao cha wavuvi kilichofanyika katika soko la samaki pangani mjini mkuu wa Wilaya ya Pangani BI ZAINABU ABDALAH amesema waziri hakuruhusu wavuvi kuvua na
nyavu za jicho la milimita nane au sita hivyo ni vyema wavuvi wakafuata sheria
wakati viongozi wakilibeba suala hilo na
kumfikishia waziri mwenye dhamana ya uvuvi.
‘’Nimesema
nafunga safari naenda Dodoma, lengo yale ambayo tunaweza kumuomba waziri atumie
busara katika kipindi hiki cha mpito hadi july 1 basi tumuombe na kama mengine
tunaweza kuyamaliza basi tuyamalize lakini hili lazima tumshirikishe waziri
mwenye dhamana kwanza kwasababu hatuwezi
kuona wananchi wetu wanateseka, biashara hazifanyiki maisha magumu tutakuja
kunyoosheana vidole watu watakapo kwama kuchangia kwenye masuala ya
kimaendeleo;
‘’Kwa
hiyo sio kwamba haya tunayamaliza hapa hapana kuna vitu Mkuu wa Wilaya tu
hawezi kuvibadili na ukilinganisha kuwa jambo lenyewe liko kisheria’’
BI ZAINABU amesema suala la faini za makosa ya uvuvi
linawaumiza wananchi wa hali ya chini kwani wanachi wengi mitaji yao ni midogo hivyo
ameahidi kulifikisha kwa waziri wa uvuvi.
‘’Kiuhalisia
sisi kama viongozi bado wananchi wetu wanaumi na hizi faini za milioni tano
kwakweli nisiwe muongo mimi mwenyewe nachangisha pesa ya matofali shilingi
elfusaba miatano lakini shida ninayoipata simwambii mtu,hali ni ngumu sana kwa
hiyo mimi nataka niwaahidi hili la faini tutaenda kuzungumza na waziri’’
Aidha BI Zainab
amewataka wananchi kutozichukua
kero za wavuvi kama ajenda za kisiasa kwani kufanya hivyo si sahihi na kuwataka wananchi kutofanya siasa kwenye
mambo ya msingi.
BI Zainab amewataka wavuvi kusubiri majibu kutoka
Wizarani ili kujua endapo wataruhusiwa kuvua na nyavu za jicho la milimita 8 au
la……
No comments