KIKUNDI CHA LENGA MBALI PANGANI CHADHAMIRIA KUWAKOMBOA VIJANA MASHULENI



 (Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha Lenga Mbali Bwana Keneth Patrick akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Funguni iliyopo Pangani Mjini wakati walipotembela shule hiyo kwa lengo la kuelimisha vijana kuhusu umuhimu wa elimu rika)

Katika kuhakikisha vijana waliayani Pangani wanainuka na kuzifikia ndoto zao za kimaisha, baadhi ya vijana wilayani humo wameungana na kuanzisha  kikundi chenye dhima ya kuwapatia elimu rika vijana hao kwa lengo la kujitambua.

Akizungumza na Pangani Fm mwenyekiti wa kikukundi hiko chenye jina la LENGA MBALI, Bwana Keneth Patrick amesema kuwa  kilicho washawishi kuanzisha kikundi hiko ni kutokana na kuona vijana wengi hawatimizi malengo yao kutokana na vikwazo mbali mbali, huku wengine wakijikita katika tabia  zisizokubalika katika jamii  hivyo  wameamua kuwafikia vijana hao kwa kuanzia mashuleni ili kuwapa uwelewa juu ya  elimu rika.

’Ni kwa ajili ya vijana au watoto wa rika la chini, kwa hiyo tumesajili kikundi na kikundi chetu kinaitwa lenga mbali, kwa lengo la kuwapatia elimu rika, tukikusudia kutoa elimu mashuleni juu ya mahusiano na jinsi ya kuepuka athari za kutumia pombe mashuleni, madawa ya kulevya, mimba katika umri mdogo na mahusian,  mashuleni kuna shida hiyo, wanafunzi hawafikii malengo na hata ukiangalia habari ya matokeo wanafunzi wengi hawafanyi vizuri na anaporudi mtaani anafanya nini ili kujikwamua na kuhakikisha tunafanyikisha maendeleo ya kijana mmoja mmoja’’ Amesema Keneth Patrick.

 (Katibu wa kikundi cha Lenga Mbali Bwana Leonard Komba akizungumza na wanafunzi wa sekondari ya Funguni)


Akizungumzia lengo la kikundi hicho Katibu wa kikundi cha LENGA MBALI Bwana Leonald Komba ametanabaisha kuwa ni kuwarudisha vijana katika kuzifikia ndoto zao huku akiongeza kuwa wanategemea kikundi hiko kiwe na ofisi yake hivi karibuni.
  
’Kwa hiyo lengo letu sisi ni kuwarudisha vijana au watoto katika mstari na lengo walilotarajia katika maisha yao ya kesho na kesho kutwa  ili wameze kufanikiwa katika maisha, tunategemea baadae tuweze kuwa na ofisi yetu, tutaanza katika shule ya sekondari Funguni leo majira ya saa 5 asubuhi mnamo tarehe 2/2/2018 na baada ya hapo tutafika hadi shule ya msingi Pangani ili kufikia walimu waliokuwepo pale na wanafunzi’’ Amesema Komba. 



Viongozi hao wamesema kuwa, kikundi cha Lenga Mbali kimebeba kauli mbiu isemayo OKOA NA TENGENEZA KESHO YAKO.

No comments

Powered by Blogger.