Wanafunzi wa shule ya msingi Pangani wilayani Pangani wameishukuru serikali na walimu wao kutokana zoezi la uendeshaji wa kampeni ya unyweshaji wa dawa za minyoo tumbo lililoendeshwa shuleni hapo.
Wakizungumza na pangani fm radio mara baada ya kunywa dawa hizo baadhi ya wanafunzi wamesema kuwa wamejisikia furaha na kuwashauri wazazi kuwapeleka watoto wao katika shule zilizo karibu ili wapatiwe dawa.
Kwa upande wake Mwalimu wa afya katika shule ya Msingi Pangani bi MWAJUMA KHAMISI amesema kuwa zoezi la ugawaji wa dawa za minyoo tumbo limekwenda vizuri na hakuna madhara yaliyojitokeza katika zoezi hilo na kuongeza kuwa kinachozingatiwa katika ugawaji wa dawa hizo ni umri.
Zoezi hilo la kampeni ya ugawaji wa dawa za minyoo tumbo kwa watoto wa umri wa miaka 5 mpaka 15 limefanyika katika shule zote za msingi wilayani pangani.
Ambapo kwa watoto wasioandikishwa shule, au ambao hawasomi shule wenye miaka 5 mpaka 15 wametakiwa kupelekwa katika shule za jirani ili kupata kinga tiba ya minyoo tumbo.
No comments