Waandishi wa habari wa redio Pangani fm kupitia shirika la Uzikwasa wamefurahi kupata mafunzo ya uchaguzi yatakayowaongoza katika kufuatilia habari za uchaguzi kwa umahiri pamoja na mbinu za kuiwezesha jamii kutambua sheria za uchaguzi ili waweze kupata viongozi bora.
Wakizungumza wakati wa mafunzo ya hayo leo hii katika ukumbi wa Pangarithi baadhi ya waandishi hao wamesema kuwa wamejifunza mambo mengi yatakayowaongoza kuandika habari za uchaguzi kwa usahihi zaidi pamoja kutoa hamasa kwa wananchi kufahamu masuala ya uchaguzi ili waweze kuwachagua viongozi bora.
Kwa upande wake Bi Rose Haji Mwalimu ambaye ni mkufunzi wa mafunzo hayo na pia mshauri wa Radio Jamii kutoka shirika la UNESCO amesema kuwa waandishi hao wamempa moyo kutokana na kuyapokea vizuri masomo hayo.
Mafunzo hayo ya siku tatu yamefadhiliwa na Baraza la habari Tanzania (MCT) ambao wametoa kipaumbele kwa waandishi wa habari wa kituo cha redio Pangani fm yatafikia tamati Jumamosi ya tarehe 25 mwezi huu.
No comments