VIJANA PANGANI WANUFAIKA NA MAFUNZO YA SDGs
Vijana takribani mia moja (100) kutokea wilayani
Pangani mkoani Tanga wamepatiwa mafunzo kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu
huku wakifanya idadi hiyo kufikia elfu Sitini (60,000) kwa waliopatiwa mafunzo kwa
nchi nzima.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari kutoka Kituo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa Didi Nafisa, wakati akizungumza na kituo hiki
katika mazungumzo maalum ndani ya Studio zetu.
Awali Afisa habari huyo kutoka kituo cha habari cha
Umoja wa Mataifa, ameanza kwa kumnukuu mwakilishi Mkazi Umoja wa Mataifa Alvaro
Rodriguez kwamba namna gani vijana wa Pangani watasaidiwa licha ya utofauti wao
wa kifikra, mitazamo na shughuli zao.
Amesema kuwa wanatembea Duniani kuwaambia vijana
kuhusu SDGs yaani Malengo ya Maendeleo endelevu ya Dunia, pamoja na kuwaelezea
ujumbe wa matumaini, iwapo malengo ya Dunia yatafanyiwa kazi.
“Alvaro anasema kwa miaka 15 ambayo imepita Umoja wa
Mataifa umekuwa ukizungumzia Malengo ya Milenia na hivi sasa tunazungumzia
Malengo ya Dunia, lakini utofauti uliopo tumeona kwamba wakati wa Malengo ya
Milenia haikuwa ikifahamika vizuri malengo haya ni kitu gani hasa kwa jamii na
ndio maana sasa tulivyofika katika Malengo haya ya Dunia tunatembea tukiwaambia
vijana kuhusu malengo ya dunia na ujumbe wa matumaini ambao malengo hayo
umeubeba, kwamba Dunia ni namna gani inaweza ikawa huko mbeleni iwapo malengo
ya dunia yatafanyiwa kazi"
Ameongeza kuwa “Pia mfumo ambao tunautumia wakati wa
kufundisha vijana, ni kwamba watakuwa wanatumia elimu waliyoipata kuwaelezea
wengine kwa kujitolea, watakuwa wanajitolea kuwaelezea wengine kwamba malengo
ya dunia ni kitu gani, tunatumaini kwamba iwapo wataweza kujitolea na
kuwaelezea wengine ujumbe huu utasambaa na kuwafikia watu wengi zaidi”. Amesema
Mwakilishi Mkazi Umoja wa Mataifa
Bi. Nafisa amesema kuwa licha ya kwamba hawajawahi
kufika Tanga kwa ujumla, lakini vijana zaidi ya elfu sitini tayari
wameshawafikia nchini, hivyo wamepania kuwafikia watu wote ili kuhakikisha
hakuna anayeachwa nyuma.
“Tangu tulipoanza mwaka 2016 mpaka sasa hivi
tumeshatoamafunzo kwa takribani zaidi ya vijana 60,000 Tanzania, kwasababu
hatujawahi kufika Pangani na Tanga kutoa mafunzo hayo hii itakuwa ni mara ya
kwanza lakini tumeshatembea zaidi ya mikoa kumi na tumekuwa tukitembea
mashuleni, vyuoni tukiongea na vijana ambao tunasema wako nje ya mfumo wa elimu
(Youth out school), tumeongea na asasi
mbalimbali”.
Amesema “Kwahiyo tunajaribu kufikia kila mtu
kwasababu kauli mbiu ya malengo ya dunia inasema (Leave
No One Behind) ni kuhakikisha kwamba hakuna mtu ambaye anayeachwa nyuma.
Kwasababu katika moja ya lengo ya malengo ya Dunia ni kuhakikisha kila mtu
anafahamu, na inatarajia kwamba kila mtu ataweza kuyafikia. Kila mtu kila nchi itaweza
kuyatimiza, na kuweza kuyatimiza ni lazima tuhakikishe kila mmoja anafahamu “hakuna
anayeachwa nyuma”.
Kwa upande wake Bi Rebeca Gyumi ambaye ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Msichana Initiative, amezungumzia namna ambavyo mpaka
sasa vijana na kila mtu anavyoshiriki kutekeleza malengo ya kidunia aidha kwa
kujua ama hata bila kujua.
“Unajua malengo ya maendeleo endelevu ni namna tu
ambavyo serikali, kwasababu ukiangalia umoja
wa mataifa ni serikali hizi zimeamua kuungano, ziliamua tu kuweka maneno ili
kusema haya ndiyo malengo yetu 17 lakini kimsingi sisi hapa wote kwa namna moja
au nyingine tulishakuwa tayari tunafanya vitu vinavyoendana na moja ya malengo
yale”.
Mafunzo kwa vijana wilayani Pangani umemkutanisha
pia mwakilishi Mkazi Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez ambaye huu ni ujuo wake
wa pili, ambapo pamoja na mambo mengine
amezungumza na mabinti Wilayani humo ili kujua changamoto zao na namna ya
kuwasaidia kufikia kwa pamoja Malengo ya Maendeleo Endelevu.
Bwana Alvaro Pangani, ameambatana na Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Msichana Initiative Bi Rebeca Gyumi pamoja na baadhi ya
wawakilishi kutoka Ubalozi wa China hapa Nchini.
Mwenyeji wa mafunzo hayo ni Mkuu wa wilaya ya
Pangani Mheshimiwa Zainab Abdallah Issa pamoja na viongozi wengine wa
kiserikali pamoja na halmashauri ya wilaya ya Pangani.
No comments