Wenza kutoka katika vijiji mbali mbali wilayani Pangani mkoani Tanga wamendelea kupata mafunzo ya namna ya kujadiliana na kuwezeshana katika ndoa, ili kuepukana na migogoro katika ndoa pamoja na masuala ya ukatili ndani ya ndoa.
Wenza hao Wakizungumzia mafunzo hayo wamesema kua wamejifunza mambo mengi ikiwemo kuacha usaliti na mfumo dume huku wakijona katika mambo ambayo yalikua yakiua ndoa zao.
Aidha wanandoa hao wameongeza kua wanazidi kupambanua namna za kuchukua hatua kutokana na maisha ya ndoa walio kua wakiishi hapo awali na kuahidi kuyafanyia kazi.
Kwaupande wa wawezeshaji wa mafunzo hayo bi SALVATA KALANGA amesema Nifuraha kubwa kwao kama muwezeshaji kuona wenza wenza wameyapokea mafunzo hayo huku wakizungumza na mambo yao mbali mblia ikiwa na maana ya kujimulika wao wenyewe huku wakiyaona mafunzo hayo kua ni tiba kwao.
Mafunzo hayo yameingia siku ya pili kwa wanandoa kutoka vijiji tofauti tofauti yakiwauhusisha wanadoa 54 huku yakiwa na lengo la “kujadiliana na kuwezeshana ili kuona kwa pamoja namna matumizi mabaya ya madaraka na mifumo ya jamii tuliyorith au tabia kandamizi zinavyo weza kuathiri maisha ya tunaopendana pia familia zetu”
No comments