TUMERUDI

Baada ya kukaa kimya kwa muda merefu, hatimae kituo cha redio Pangani Fm kimerudisha utoaji wa taarifa zake kwa njia ya mtandao, kufuatia kuwepo kwa sheria mpya ya mawasiliano.

Pangani Fm ilifunga utoaji wa taarifa zake kupitia blog hii April 15, 2018, na kuomba radhi mashabiki wake kuwa haitakuwa inatoa taarifa yoyote mpaka pale itakapopata leseni, suala ambalo imefanikiwa.

Ikumbukwe kuwa serikali imeweka utaratibu wa malipo kupitia wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kwenye Electronic and Postal Communications (Online Content).

Kuanzia tarehe ya leo Februaly 6, 2019 Pangani itaendelea kutoa taarifa zote kwa mashabiki wake, sambamba na kusikiliza matangazo yetu moja kwa moja kupitia blog hii.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kipindi ambacho hatukuwa hewani hapa.

2 comments:

  1. Nawapongeza sana Pangani FM kwa hatua nzuri mliyopiga kuhabarisha umma masuala mbalimbali yanayojiri katika jamii ya wilaya ya Pangani,Mkoa wa Tanga, Tanzania na Duniani kote kwa ujumla, sasa nawapata vizuri kabisa kupitia Radio Bora katika Mkoa wa Tanga (Pangani FM), pigeni kazi, hata ikiwezekana basi "Punda afe Mzigo ufike" safi sanaa

    ReplyDelete

Powered by Blogger.