HIVI NDIVYO MAZISHI YA ALIYEKUWA MWENYEKITI CCM WILAYA YA PANGANI YALIVYOKUWA.


Mwili wa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Pangani mkoani tanga Mzee Hamisi Mnegero aliyefariki jana wakati wa swala ya asubuhi katika kijiji cha Kwakibuyu umezikwa leo katika makaburi ya familia yao kitongoji cha Shirikishoni kilichopo kijiji cha Mikocheni wilayani Pangani. Mazishi hayo yamehudhuriwa na mamia ya watu kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo viongozi wa vyama vya siasa na serikali wa ndani na nje ya mkoa wa Tanga. NI wakinamama wakiongoza maombolezo katika shughuli ya kumpeleka katika makazi ya milele mwenyekiti huyo wa CCM aliyekihudumia chama hicho kwa misimu mitano mfululizo. Wakizungumza katika shughuli ya mazishi ya mwenyekiti huyo viongozi kutoka maeneo mbalimbali wamezungumzia namna walivyoguswa na msiba huo huku wakihimiza viongozi kufuata mambo mazuri aliyoyafanya mwenyekiti huyo wakati alipokuwa madarakani. Nao baadhi ya viongozi wa chama cha CUF wilaya ya Pangani wamelezea uongozi wa mwenyekiti huyo alipokuwa madarakani ulikuwa ni uongozi usio wenye kubagua. Nikiwa katika shughuli hii ya mazishi nimezungumza na wakazi waliohudhuria katika mazishi wakisema mzee mnegero atakumbukwa kwa mambo mengi mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake. Pamoja na kushika nyazifa ya Uwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Pangani Mzee hamisi mnegero wakati wa uhai wake alikuwa ni Shehe Mkuu kata ya Kipumbwi mpaka umauti unamfika na ameacha mke mjane mmoja, watoto nane, wajukuu 21 na vitukuu vinne, Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema pepon Amin.

No comments

Powered by Blogger.