MASAIKA WAAZIMIA HIVI KUHUSU UKATILI


Viongozi wa kamati ya kudhibiti ukimwi jinsi ana uongozi pamoja na kamati ya shule ya msingi masaika wilayani pangani wamesema kuwa wataendelea kushirikiana kwa hali na mali ili kuendelea kuyafichua matukio ya ukatili yanayotokea katika kijiji hicho. Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wenzie wa kamati ya vmac pamoja na kamati ya shule bwana PAUL EDWARD ameeleza kuwa kama viongozi wana mambo mengi ya kuyafanya ikiwamo kutambua matatizo ya ukatili na kuyawekea mikakati ya namna ya kuyatokomeza. “kuna vitu ambavyo tunapaswa kuvifanya ila hatukuvifanya, swala la kwanza ni kuyatambua yale matatizo ya kijinsia au ya ukatili na kuyaandaa katika mpango kazi na kuyaweka katika fomu na kupelekeka sehemu husika ili kukaa kikao na kuyajadili ,swala la pili ambalo tunatakiwa kuyafanya sisi kama jamii, kamati ya shule pamoja na vimac ni kutambua matatizo madogo madogo ya wanafunzi mfano chumba cha kujistiri kwa watoto wa kike katika shule yetu hili ni tatizo na tutalichukua sisi kama wajumbe na kuliwekea mkakati ili kufuatilia suala hili”

No comments

Powered by Blogger.