Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU imebainisha mianya 35 ya rushwa iliyojitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka 2014.
Akizungumza katika kikao cha uelimishaji juu ya vitendo vya rushwa vinavyojitokeza wakati wa uchaguzi wa serikali za Mitaa Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya pangani bwana Joseph Paul amesema kuwa pamoja na jitihada za serikali katika kusimamia chaguzi mbalimbali nchini vitendo vya rushwa vimeendelea kuongezeka katika chaguzi mbalimbali.
Bwana Paul amesema kuwa sababu haswa ya kuwasilisha utafiti huo ni kutoa nafasi kwa wananchi na wadau mbalimbali wa uchaguzi kujifunza na kupata tahmini kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Tafiti hiyo imeonyesha kuwa ukiukwaji wa sharia na miongozo umetoa mianya ya rushwa katika uchguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka
Kikao hicho likihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali ngazi mbalimbali,wawakilishi wa taasisi za kidini, kijamii, vyama vya siasa pamoja na wawakilishi kutoka kamati za ulinzi na usalama.
No comments