DAS PANGANI APONGEZA UFAULU WA SEKONDARI
Katibu tawala wilayani Pangani Mwalimu HASSANI NYANGE ametoa
pongezi kwa waratibu elimu kata na halmashauri yote kwa matokeo mazuri ya
kidato cha nne mwaka 2018 katika shule ya
sekondari Bushiri.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo
Mwalimu NYANGE alisema.
‘’kwanza kabisa niwapongeze ndugu zetu wa idara ya elimu,
pamoja na halmashauri kwa nafasi ambayo tumepiga naa hii inaonyesha kabisa ni
kwamba japo kuwa hatukutarajia kuwa wa hamsini, lakini mipango mikakati
imeshaanza, nafikiri tulikubaliana. Waheshimiwa madiwani niwaombe tutembelee
shule zetu tuangalie kama waratibu kata wanafika na kama wanafanya follow up ya
watoto wetu. Wao wanajukumu kubwa la kusimamia shule zetu za msingi na
sekondari lakini pia wanawajibika kuwapa taarifa ya yanayoendelea kule yaani
isitokee mapungufu ya walimu au changamoto za shule na wewe ukaja kuzisikia
hapa wakati yeye yupo na wewe kule, kwa hiyo niwaombee muwabane na
muwafuatilie’’
Aidha Mwalimu
Nyange amewasisitizia madiwani
hao kusaidia suala la chakula mashuleni kwani suala hilo linawagusa wao moja
kwa moja sambamba na kutoa pongezi kwa wadau wa shule ya sekondari bushiri kwa
kuanzisha bweni mapema kwa wanafunzi wao.
NYANGE amesema shule ya bushiri ni shule ya kwanza ya
serikali iliyofanya vizuri na malengo ya halmashauri ni kuwa kumi bora, na
kumtaka diwani wa kata ya Mwera kuupokea mpango wa kidato cha tano unaotarajiwa
kuanzishwa katika kata yake.
No comments