TAKRIBANI SHILINGI MILIONI 16 ZAHITAJI KUFANIKISHA MRADI WA MAJI CHOBA



Tabribani milioni Kumi na sita laki tatu na elfu kumi na mbili zinahitajika  ili kufanikisha mradi wa maji katika kitongoji cha choba kijiji cha boza wilayani PANGANI.
 
Hayo yamezungumzwa na muhandisi wa maji wilayani Pangani  Bwana WILSON NOVATH Ambapo amesema kuwa  fedha hizo zitawezesha kutoa maji katika kitongoji cha Mnazi mmoja hadi katika kitongoji cha choba.

Akitoa ufafanuzi wa matumizi wa fedha hizo Bwana Wilson ameongeza kuwa Vifaa vyote vitagharimu milioni kumi na moja, laki tatu na elfu sabini na mbili huku nguvu kazi na vifaa vingine vikikamilisha idadi ya fedha iliyopangwa.




Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha boza Bwana Shabani Sufiani Amesema ili kupunguza Gharama Katika bejeti hiyo, wao kama wakereketwa wakubwa wa maji wakitongoji cha choba, watachangia Ardhi itakayopita mabomba hayo pamoja na kufikia mitaro.
Adha ya maji imekuwa kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa kitongoji cha choba huku kilio hiko kikioneka kinaanza kupungua kutokana na mikakati endelevu ya serikali kuyafikisha maji katika kitongoji hiko.

No comments

Powered by Blogger.