WANANCHI WILAYANI PANGANI WATAKIWA KUJITOLEA KUCHANGIA DAMU



Wito umetolewa kwa wananchi wa wilaya ya pangani kuwa na utaratibu wa kuchangia damu ili kupunguza vifo na adha mbali mbali zinazotokana na  upungufu wa damu wilayani Pangani. 

Wakizungumza na kituo hiki mara baada ya zoezi la kuchangia damu lililofanyika katika eneo la standi ya mabasi mjini Pangani, baadhi ya wananchi wamesema kuwa kuchangia damu kutawezesha wagonjwa wenye uhitaji kuepukana na adha mbalimbali zinazojitokeza.

Mwananchi mmoja anayefahakima kama Bakari Rambazo ambaye pia ni mchangiaji wa damu katika zoezi hilo amesema kuwa kuna faida nyingi za kuchangia damu ikiwemo kuokoa maisha ya wagonjwa mbalimbali jambo linalopelekea mchangiaji wa damu kupata  thawabu kwa mwenyezi Mungu.

Naye mjumbe wa kamati ya damu salama kutoka katika hospital ya wilaya ya Pangani ambaye ndiye aliyeendesha zoezi hilo Bwana Peter Mshabaha amesema kuwa zoezi hilo limesuasua kwa kuwa wananchi wengi hawana muamko wa kuchangia damu hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwani zoezi hilo pia linasaidia mchangiaji kujua afya yake.

Zoezi la uchangiaji damu limekuwa likihamasishwa nchini nzima kupitia serikali ili kuokoa maisha ya wagonjwa hususani wakina mama wajawazito na watoto.

No comments

Powered by Blogger.