HALMASHAURI YA PANGANI YAANZA KUHAMASISHA WANANCHI UJENZI WA KITUO CHA AFYA MWERA



Halmashauri ya wilaya ya Pangani kupitia idara ya afya imeanza uhamasishaji wa ukarabati na ujenzi wa kituo cha afya cha Mwera kwa kuvishirikisha vijiji vya jirani ikiwa ni pamoja na kijiji cha Langoni wilayani humo.

Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mwera na Langoni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Pangani  Bwana Daudi Mlahagwa ameeleza kuwa ujenzi huo utazingatia mfumo wa force account hivyo wananchi wa vijiji hivyo wanatakiwa washiriki kwa kujitolea nguvu kazi.

‘’Nini ambacho watu wanatarajia na serikali inatarajia ni kuona kwamba hii fedha inatumika kwa utaratibu ambao umeelekezwa na serikali kwa hiyo mtaona kwamba muda tuliopewa sisi ni mfupi unaitaji sana ushirikiano, kwa hiyo tuombe tu kwamba ushiriki wa wananchi ni kitu cha msingi na  ni lazima tufanye kwa muda ambao umeelekezwa’’ amesema Bwana Mlahagwa.



Nao wananchi wa vijiji hivyo hususani wakina mama wamesema kuwa  wameupokea mradi huo na kuahidi kushiriki kwa dhati kwenye zoezi hilo la kujitolea nguvu kazi ili kuepuka adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya afya.

‘’Sisi wananchi wa kijiji cha Langoni tumeupokea vizuri kwa sababu mimi mwanangu alishawahi kuzaa eneo la Bweni kutokana na changamoto ya feri lakini kwa sasa tunaafurahia kweli tunaomba tu mradi uanze hata sasa hivi na tutatoa ushirikiano kwa nguvu zote.’’ Amesema mmoja wa wananchi.



Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Pangani Bwana Juma Mfanga  mbali na  kutaja miundombinu itakayoongezwa katika kituo hicho ikiwemo jengo la upasuaji, maabara, chumba cha kuhifadhia maiti, wodi ya wazazi, pamoja na wodi ya watoto pia jingo hilo litazingatia  mgawanyo wa kazi  kwa  kila kijiji.

‘Kwa hiyo katika mgawanyo wetu wa kata tunaweza tukasema vitongoji vyetu vya Mzambarauni kazi yao itakuwa kututafutia mawe kisha wayaweke hapa na sisi tutakwenda kutafuta usafiri wa kuyapakia ili yatumike kwenye ujenzi, nah ii ndo tunasema kujitolea’’ Amesema Bwana Mfanga.

Mradi huo ambao umetengewa shilingi milioni 400 kupitia ofisi ya rais TAMISEMI utatekelezwa kwa siku tisisni tangu fedha hizo zilipoingizwa kwenye akaunti.

No comments

Powered by Blogger.