AJERUHIWA NA PANGA WAKATI AKIIBA MIHIGO HUKO MADANGA
Kijana
mmoja mkazi wa kijiji cha Madanga
Wilayani Pangani amejeruhiwa kwa kukatwa
na Panga katika mkono wake wa kulia baada ya
kukutwa aking’oa Mihogo shambani kwa Bwana MWINYIHAJI KARAFUU bila idhini
ya mmiliki wa shamba hilo.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda
wa polisi wilaya ya Pangani Bi
CHRISTINA MUSYANI amesema kuwa
mnamo tarehe 5 mwezi huu wa pili majira ya saa tisa Alasiri Bwana MDABIDA
CHAMBEGA mkazi wa kijiji cha Madanga, alijeruhiwa baada ya kukutwa akiiba Mihogo shambani kwa Bwana KARAFUU
yenye thamani ya shilingi elfu sita.
“Ni kweli
taarifa hizo zipo, ambapo tukio hilo lilitokea tarehe 5 February 2018 majira ya
saa Tisa na robo hivi Alasiri, kwamba ndugu Mdabida Chambega (30) ambaye anaishi
Madanga alijeruhiwa kwa kukatwa katika mkono wake wa kulia kwa kutumia Panga na
ndugu Mwinyihaji Karafuu”. Amesema Kamanda huyo wa Polisi Pangani na kuongeza
kuwa.
“Huyu Mdabida
alikuwa katika shamba la Mihogo la Bwana Mwinyihaji alikuwa akivuna bila
kuruhusiwa ina maana alikuwa akiiba, hivyo ndugu Mwinyihaji alipogundua kuna
mtu anavuna katika shamba lake akamshambulia kwa Panga, lakini Mihogo ambayo
wakati huo ameshaing’oa ilikuwa na thamani ya shilingi elfu sita”.
Aidha Bi
Musyani amewataka wananchi kuwa waaangalifu na kutii sheria za nchi
zilizowekwa, pamoja na kuacha kujichukulia sheria mkononi.
“Huyo
Bwana Mdabida alikutwa anaiba Mihogo isiyo ya kwake, tunasisitizana kila siku
kutokuchukua sheria mkononi, tuwe waangalifu, kwa sababu unakuta inaibua hiyo
ya kujeruhi wakati tulikuwa na kesi ya msingi ya wizi. Sasa hapo naendelea
kusisistiza jamii ya Pangani kuwa waangalifu katika haya wasichukue sheria
mkononi”. Amesema Kamanda Musyani.
Katika
hatua nyingine Kamanda Musyani amewataka wananchi kufanya kazi na kutumia
rasilimali ardhi katika shughuli za kilimo, na kuacha vitendo vya wizi kwani
vinarudisha nyuma maendeleo.
No comments