ANASURIKA KIFO BAADA YA KUNYWA SUMU YA PANYA
Kijana mmoja mkazi wa Kitongoji cha Kimang’a B Wilayani Pangani ambaye jina lake limehifadhiwa, amenusurika kufa baada jaribio la kutaka kujiua kwa kunywa sumu ya Panya akidai kuwa maisha ni magumu.
Akizungumza na Pangani Fm Kamanda wa
Jeshi la Polisi Wilayani humo Bi Christina Musyani, amethibitisha tukio hilo na
kusema kuwa baada ya kupata taarifa kwa wasamaria wema walifuatilia suala hilo na baadae kugundua kuwa ni kweli ambapo haraka mtu huyo alikimbizwa
kituo cha Afya ili kuokoa maisha yake.
“Taarifa hii ni ya kweli sisi
tumeithibitisha kw asababu tulipata taarifa tarehe 11 mwezi huu wa pili majira
ya alfajiri, kwamba kuna kijana katika kitongoji cha Kimang’a B alikuwa
amejaribu kujiua usiku wa tarehe 10 majira ya saa tano na nusu usiku akiwa
ndani ya nyumba yake” Amesema kamanda Musyani na kuongeza kuwa….
“Alijaribu kujiua kwa kunywa sumu ya
Panya lakini tunashukuru Mungu kwamba hakuweza kufariki, ndugu yake aliweza
kumgundua mapema na kutoa hizo taarifa na akakimbizwa katika kituo cha afya
akapata huduma”.
Aidha Kamanda Musyani amesema kuwa mtu
yoyote anae jaribu kudhuru mwili wa mtu mwingine ama mwili wake, ni kosa kisheria
na hivyo kutokana na hilo kijana huyo anashtakiwa na atapelekwa Mahakamani,
huku akiwahimiza vijana kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujikimu kimaisha.
“Mimi
nitoe wito kwa vijana na rika lote kujiua sio suluhisho, tujibidiishe katika
kazi na tufanye kazi sahihi itayotambulika yaani halali ili upate kipato uweze
kujikimu, mbona tuna ardhi ya kutosha hebu tuitumie kwa maslahi mapana ya
maisha yetu”. Amesisitiza kamanda huyo
No comments