MAHAKAMA PANGANI YAADHIMISHA SIKU YA SHERIA NCHINI
Mahakama wilayani Pangani kwa kushirikiana na
wadau mbali mbali wameungana katika kuadhimisha siku ya sheria nchini iliyokuwa
imebeba kauli mbiu isemayo ‘Matumizi Ya Tehema Katika Utoaji Haki Kwa Wakati,’
shughuli iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi hizo zilizopo Pangani Mjini.
Akizungumzia kauli mbiu hiyo Kaimu Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Pangani, Bi Crisencia Kisongo amesema kuwa,
mfumo wa Tehama utasaidia kuhifadhi taarifa za mashauri za kimahakama na utarahisisha upatikanaji wa majalada huku
ukisaidia upatikanaji wa malalamiko kwa wateja.
‘'Mahakama ndio chombo pekee nchini ambacho kina
jukumu la kutoa haki , Mahakama kama ilivyo vyombo vingine au mihimili mingine
haiko nyuma kwenye matumizi ya Tehama, tayari imeshaanza na tayari inaendelea
na matumizi ya hiyo teknolojia ya habari na mawasiliano’’ Amesema Bi Crisencia.
Bi Crisensia pia amewataka wananchi wilayani Pangani
kutosita kuuliza kwa wataalamu wa sheria juu ya maswala mbali mbali ya kisheria.
‘’Tuseme tu watumishi wote wa kimahakama, mahakimu
na viongozi wote wapo tayari kuendelea kutoa elimu kuhusiana na shughuli mbali
mbali zinazofanywa na mahakama wakati wote tunawakaribisha” Amsemema Bi Kisongo.
Kwa upande wa wananchi waliojitokeza katika kilele
hicho hawakusita kutoa maoni yao kwa vyombo vya sheria wilayani humo huku
wakiviasa kutenda haki.
‘’Siku ya sheria leo nashukuru imekwenda vizuri na
kuna baadhi ya vipengele ambavyo tumejaribu kuhamasishwa au kutusaidia sisi
ambao ni watu wa chini na kwamba mambo ya kisheria tulikuwa tunayaona ni mageni
na tunaimba mahakama iwe inatenda haki’’ Amesema mmoja wa wananchi.
Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo ya sheria wilayani
Pangani ni Bwana Peter Mabuga ambaye ni katibu tawala wilayani Pangani, amewataka
wananchi kuchukua hatua kwa maafisa wa Mahakama wanaowaomba rushwa pamoja na
kuwaasa watumishi wa Mahakama kutenda haki.
‘’Tusiishie kulalamika, chukueni hatua dhidi ya
maofisa wa mahakama ambao wanakiuka maadili ya kazi zao wanaojihusisha na
vitendo vya rushwa badala ya kulalamika kimnywa kimnywa tu.’’ Amesema Mabuga.
Maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini
Tanzania hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa mwezi wa pili, ambapo kwa mwaka huu yaliobeba
kauli mbiu isemayo MATUMIZI YA TEHEMA
KATIKA UTOAJI HAKI KWA WAKATI.
No comments