KIKUNDI CHA LENGA MBALI PANGANI CHADHAMIRIA KUWAKOMBOA VIJANA MASHULENI
(Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha Lenga Mbali Bwana Keneth Patrick akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Funguni iliyopo Pangani Mjini wakati walipotembela shule hiyo kwa lengo la kuelimisha vijana kuhusu umuhimu wa elimu rika)
Katika kuhakikisha vijana waliayani Pangani
wanainuka na kuzifikia ndoto zao za kimaisha, baadhi ya vijana wilayani humo
wameungana na kuanzisha kikundi chenye
dhima ya kuwapatia elimu rika vijana hao kwa lengo la kujitambua.
Akizungumza na Pangani Fm mwenyekiti wa kikukundi
hiko chenye jina la LENGA MBALI, Bwana Keneth Patrick amesema kuwa kilicho washawishi kuanzisha kikundi hiko ni
kutokana na kuona vijana wengi hawatimizi malengo yao kutokana na vikwazo mbali
mbali, huku wengine wakijikita katika tabia
zisizokubalika katika jamii
hivyo wameamua kuwafikia vijana
hao kwa kuanzia mashuleni ili kuwapa uwelewa juu ya elimu rika.
‘’Ni
kwa ajili ya vijana au watoto wa rika la chini, kwa hiyo tumesajili kikundi na
kikundi chetu kinaitwa lenga mbali, kwa lengo la kuwapatia elimu rika,
tukikusudia kutoa elimu mashuleni juu ya mahusiano na jinsi ya kuepuka athari
za kutumia pombe mashuleni, madawa ya kulevya, mimba katika umri mdogo na mahusian,
mashuleni kuna shida hiyo, wanafunzi
hawafikii malengo na hata ukiangalia habari ya matokeo wanafunzi wengi
hawafanyi vizuri na anaporudi mtaani anafanya nini ili kujikwamua na
kuhakikisha tunafanyikisha maendeleo ya kijana mmoja mmoja’’ Amesema Keneth Patrick.
(Katibu wa kikundi cha Lenga Mbali Bwana Leonard Komba akizungumza na wanafunzi wa sekondari ya Funguni)
Akizungumzia lengo la kikundi hicho Katibu wa
kikundi cha LENGA MBALI Bwana Leonald Komba ametanabaisha kuwa ni kuwarudisha
vijana katika kuzifikia ndoto zao huku akiongeza kuwa wanategemea kikundi hiko
kiwe na ofisi yake hivi karibuni.
‘’Kwa
hiyo lengo letu sisi ni kuwarudisha vijana au watoto katika mstari na lengo
walilotarajia katika maisha yao ya kesho na kesho kutwa ili wameze kufanikiwa katika maisha, tunategemea
baadae tuweze kuwa na ofisi yetu, tutaanza katika shule ya sekondari Funguni leo
majira ya saa 5 asubuhi mnamo tarehe 2/2/2018 na baada ya hapo tutafika hadi
shule ya msingi Pangani ili kufikia walimu waliokuwepo pale na wanafunzi’’
Amesema Komba.
Viongozi hao wamesema kuwa, kikundi cha Lenga Mbali
kimebeba kauli mbiu isemayo OKOA NA TENGENEZA KESHO YAKO.
No comments