MBUNGE WA PANGANI AENDELEA NA ZIARA WILAYANI HUMO
Mbunge wa Jimbo la Pangani Mheshimiwa Jumaa Hamidu
Awes leo ameendelea na ziara yake katika jimbo lake na kutoa msaada wa Mifuko
arobaini ya saruji katika shule ya chekechea ya Childrens Of Choba wilayani
humo.
Akizungumza wanafunzi na viongozi wa shule hiyo
mbunge Jumaa amesema kuwa ameamua kutoa mifuko arobaini ya Saruji kutokana na
kutambua mchango wa meneja wa shule hiyo katika kuendeleza watoto wa Pangani
katika elimu.
Kwa upande wake Meneja wa shule hiyo Bi Valeri Makgiven ameshukuru kwa
msaada huo akisema utasaidia katika kupanua ujenzi wa madarasa ya Awali katika
shule hiyo.
Hata hivyo baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika
shule hiyo wamemshukuru Mbunge huyo kwa msaada alioutoa huku wakimuahidi
watajihidi katika kujisomea ili waweze kupata mafanikio kielimu.
Mbunge wa jimbo la Pangani mheshimiwa Jumaa Hamidu
Aweso bado anaendelea na Ziara yake kutembelea vijiji vya jimbo hilo ili
kutambua changamoto zilizopo na kuzitatua kabla ya kurudi bungeni mwezi wa Tisa mwaka huu.
No comments