TAKRIBANI SHILINGI MILIONI 16 ZAHITAJI KUFANIKISHA MRADI WA MAJI CHOBA
Tabribani milioni Kumi na sita laki tatu na elfu kumi na mbili zinahitajika ili kufanikisha mradi wa maji katika kitongoji cha choba kijiji cha boza wilayani PANGANI.
Hayo yamezungumzwa na muhandisi wa maji wilayani
Pangani Bwana WILSON NOVATH Ambapo
amesema kuwa fedha hizo zitawezesha
kutoa maji katika kitongoji cha Mnazi mmoja hadi katika kitongoji cha choba.
Akitoa ufafanuzi wa matumizi wa fedha hizo Bwana
Wilson ameongeza kuwa Vifaa vyote vitagharimu milioni kumi na moja, laki tatu
na elfu sabini na mbili huku nguvu kazi na vifaa vingine vikikamilisha idadi ya
fedha iliyopangwa.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha boza Bwana Shabani
Sufiani Amesema ili kupunguza Gharama Katika bejeti hiyo, wao kama wakereketwa
wakubwa wa maji wakitongoji cha choba, watachangia Ardhi itakayopita mabomba
hayo pamoja na kufikia mitaro.
Adha ya maji imekuwa kilio cha muda mrefu kwa wakazi
wa kitongoji cha choba huku kilio hiko kikioneka kinaanza kupungua kutokana na
mikakati endelevu ya serikali kuyafikisha maji katika kitongoji hiko.
No comments