TAMAPENDO- Tamthilia Mpya Ya UZIKWASA Wilayani Pangani
Kwa mara nyingine tena shirika la UZIKWASA lililopo
wilayani Pangani limekuja na mambo mapya. Safari hii ni tamthilia ya mchezo wa
redio unaofahamika kama Tamapendo.
Lengo la tamthilia hii ni
kuonesha changamoto za vijana wawili kujiendeleza katika maisha yao katika
jamii ambapo kanuni za unyanyasaji wa kijinsia za kijamii bado zinashinda.
Tamapendo
inakuwa tamthilia ya pili ya redio kutengenezwa na shirika la UZIKWASA baada ya
mchezo wa redio wa Penye Nia…..uliopatwa
kusikilizwa na jamii nzima ya Pangani kupitia kituo cha redio cha Pangani FM,
ambacho pia kinamilikiwa na shirika la UZIKWASA wilayani Pangani.
Shirika hili pia limekuwa na utaratibu kutengeneza filamu
mbali mbali hasa kuhusu masuala ya haki na ukatili wa kijinsia. Kutokana na utafiti wa ndani kabisa filamu za
UZIKWASA zinasimulia story halisi za jamii ya Pangani na zilifanikiwa kugusa
watamazaji kwa sababu filamu hizi ni kama kioo cha changamoto zao.
Filamu hizo ni Fimbo ya Baba ambayo ilitengenezwa mwaka
2006, Chukua Pipi iliyotoka 2012
na filamu maarufu ya AISHA ya
mwaka 2015. AISHA ilifanikiwa kwa kiasi
kikubwa, siyo Pangani tu, lakini Tanzania nzima na nchi nyingi za kimataifa.
Imepata tuzo mbalimbali kimataifa kutoka tamasha za filamu maarufu USA na
Africa.
Pamoja na hayo yote, sasa shirika la UZIKWASA limekuja
tena na tamthilia ya redio inayoitwa Tamapendo.
Kama kawaidi ya filamu na tamthilia ya redio za UZIKWASA karibu waigizaji wote
hutokea Pangani.
Na ndivyo ilivyotokea kwa Tamapendo ambayo imeongozwa kwa ushirikiano na wagurugenzi wa
mchezo Chande Omar na Irene Sanga. Story
ya tamthilia hii inatokana na tafiti iliofanyika na UZIKWASA pamoja na mchango
wa wanajamii wa Pangani.
Tamthilia imetengenezwa na kuhaririwa kwenye studio ya
redio Pangani FM –Sauti ya Jamii.
Tamapendo ni kuhusu nini?
Ni story ya
vijana wawili Fatuma na Chaballa wanaokutana na dhuruba kubwa ya maisha. Wanajiona kuelemewa na mambo mazito kuhusiana
na ukatili mbalimbali na dharau kuhusiana na haki za wanawake na wasichana.
Wakati wakijinusuru kutetea upendo wao wa dhati na
kufuatilia ndoto zao katika maisha, wanajikuta kunaswa na mtego wa tamaa
unaotawala kijijini kwao.
Ni matumaini ya UZIKWASA kuwa Tamapendo ambayo tayari imeshazinduliwa, itazunguka nchi nzima ili kuwafikia
wasikilizaji wengi na kuibua mijadala.
No comments