MSEKO NA MEKA WAAHIDI KUWEKA TOFAUTI ZAO PEMBENI NA KUAMUA KUKUZA ELIMU.



Kambi ya mafunzo ya Minna Dada kwa kamati ya shule, kijiji cha Meka na Mseko imemalizika rasmi leo huku wajumbe waliohudhuria mafunzo hayo wakiahidi kufanyia kazi changamoto walizokuwa zinawakabili.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo mwenyekiti wa kijiji cha Mseko Bwana Armano Michael, mbali na kulishukuru shirika la UZAKWASA, pia amesisitiza suala la ushirikiano baina ya vijiji hivyo ambavyo awali vilikuwa na mvutano.

Nae mwenyekiti wa kijiji cha Meka Bwana Omary amewataka wajumbe wa kamat hiyo kwenda kuwaelimisha wananchi yale waliyojifunza, ili kukuza ufaulu kwa watoto wao.


Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Bi Medesta Christofa amewashauri wazazi kujitoa na kuchangia suala la chakula shuleni kama wanavyofanya nyakati sikukuu ili kuwaepusha watoto wao na mazingira hatarishi.

Mafunzo hayo yanayotolewa na shirika la UZIKWASA kwa kamati za shule za msingi wilayani Pangani hufanyika kwa siku tatu mfululizo yakiwa na lengo la kuziwezesha kamati hizo kutekeleza majukumu yao pamoja na kujiwekea mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizopo katika maeneo yao

No comments

Powered by Blogger.